Forex Trading Ni Nini

Biashara ya Forex Ni Nini

Forex Trading Ni Nini? Forex Ni Biashara Ya Ubadilishaji Wa Fedha Za Kigeni Ambayo Imeonekana Kuwa Na Mzunguko Mkubwa Zaidi Kuliko Biashara Yoyote Dunianini Kwani Inazungusha Zaidi Ya Dolla Za Kimarekani Trillion 5 Kwa Siku.

Hii Ni Biashara Ambayo Imechangiwa Sana Na Mapinduzi Ya Teknolojia Ambapo Sasa Mtu Yeyote Unaweza Ukafanya Biashara Hii Ambapo Kuna Mtandao Wa Intaneti Kama Kompyuta Na Simu Janja a.k.a Smart Phone

Kama hujui forex ni nini basi hapa ndio nitakwambia kwa undani zaidi forex ni nini

1. Forex ni kifupisho cha FOReign EXchange kwa maana ya biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni. Kama unavyoijua kazi ya Bureau de Change, ndiyo hiyo hiyo tunaifanya kwenye Forex ila hii ni ya mtandaoni.

2. Forex ni biashara halali na inafanyika ulimwenguni mwote na taasisi kubwa kubwa za kifedha na mabenki na central banks.


3. Biashara hii ni ya mtandaoni na wauzaji na wanunuzi hukutana huko soko lake ni la mtandaoni na ni la dunia nzima. Inakadiriwa kuwa, biashara hii imevutia wawekezaji ambao kwa pamoja (wakubwa na wadogo) wanatrade zaidi ya US Dollars Trilioni 5.3 kila siku!

4. Hii biashara kwa kuwa ni ya mtandaoni, ukitaka kuifanya ni lazima uwe na fedha mtandaoni. Unafungua account mtandaoni kama unavyofungua bank, unaweka fedha zako. Unazifanyia biashara na siku ukitaka kuzitoa, unazitoa mtandaoni zinakuwa cash za kutumia.

5. Biashara hii, kwa kuwa ni ya mtandaoni, unaweza kuifanyia popote! Nyumbani, chumbani, njiani, sokoni..popote!

Forex Trading Ni Nini

Unahitaji tu vitu vitatu:
a) Computer/Laptop ambayo itakusaidia kuliangalia soko na kujua muelekeo (Market Analysis)

b) Internet connection. Kwa sababu ni biashara ya mtandaoni, unahitaji kujiunga na mtandao.

c) Programu maalum yenye uwezo wa kusoma soko. Hii inaitwa Trading Platform. Hii ni software ambayo, unai-download na kui~install kwenye Computer yako. Hizi ziko nyingi sasa lakn moja maarufu ambayo inatumika sana duniani inaitwa Meter Trader 4 (MT4).

Note 1: Ni lazima uwe na Computer/Laptop na ui~install MT4 kama unafanya Market Analysis mwenyewe lakini, kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya kwa niaba yako na akakupa kile tunaita Trading Signal, sio lazima uwe nayo. Unaweza tu ukawa na simu yako au gadget yoyote ile inayoweza kuunganishwa na mtandao. Uzuri, hata MT4 nazo, zimetengenezwa mpaka za simu hivyo, unaweza kui~install katika simu na ukaendelea kutrade.

Note 2: Baada ya kutimiza hayo, kabla hujaanza KUNUNUA NA KUUZA fedha za kigeni mtandaoni, au Ku~Trade Forex, unamuhitaji mtukati anayeitwa Broker. Kwanini? Nitafafanua zaidi, lakini, kwa hapa niseme tu, ndiye anayesimama kama bank ya mtandaoni kwako. Utafungua account kwake kama unavyofungua account NMB, NBC, Equity, Exim, n.k. Utampatia taarifa zako zote rasmi, Vitambulisho vyote muhimu, Uraia, Anuani ya unapoishi,…kila kitu. Ndipo atakuruhusu kufungua account ya mtandaoni. Niwaonye wanaopenda kudanganya, hapa usijaribu, utafeli. Hapa wanahitaji taarifa zako halisi na sahihi.

Hii ni kwa sababu, hii ni biashara halali kabisa, na ni ya dunia nzima na, inakupatia kipato halali. Sasa, siku umepata faida unataka kuzitoa pesa zako, watakuambia hatukupi maana si wewe, endapo utawasilisha utambulisho mwingine tofauti na ule uliojazaga. Baada ya kuifungua account kwa Broker, unaweka hela zako humo, labda USD, GBP, JPY..utakavyo mwenyewe. Baada ya hapo, sasa upo tayari kuanza biashara.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x