Aina Ya Forex Traders Katika Soko La Forex.

Aina Ya Forex traders

Hii ni eneo muhimu sana kulijua na wewe kufanya maamuzi unataka uwe trader wa aina gani. Hivyo kabla hujaanza ni bora kujitathmini wewe ni mfanyabiashara wa aina gani na utumie njia zipi katika kufanya biashara yako.


SCALPER TRADER
Huyu ni mfanyabiashara anaekuwa katika soko kwa mda mfupi sana. Mara nyingi anaingia na kutoka katika trade na dakika kadhaa tu. Kivutia kikubwa kwa trader wa aina hii huona faida au hasara ndani ya mda mfupi tu.

Msingi mkubwa wa scalper ni kuwa na uwezo wa kufikiri haraka na kuweza kumantain pressure. Kulingana na mda mfupi wa fursa scalper huamua aingie katika hio fursa au aache

DAY TRADER
Huyu ni trader ni yule ambae huingia katika trade siku husika na kutoka katika trade siku hio hio.Tofauti na scalper, yeye huingia katika trade na kuisubiri ndani ya dakika 30 au saa. Uzuri wa kuwa day trader ni mda wa kutosha wa kufanya zako analysis.

Mara nyingi huwa na mda maalum wa kuingia katika trades zake. Na mda ukifika wanasubiri fursa ijitengeneze na kuingiza trades zao, hutumia dakika 30, saa moja mpaka saa 4 timeframe kufanya analysis zao.


SWING TRADER
Hawa ni traders wanaofanya biashara kila siku…. kwa kua kila siku kunakuwa na nafasi za mtiririko/swings katika soko. ukitokea mtririko wa kupanda wanapanda nao.. ukitokea wa kushuka wanashuka nao. Hawa wanafocus sana katika kuangalia mtiririko wenye asili ya uimara zaidi, na mara nyingi hutokea katika kufunguliwa kwa soko la london (London open) na New York open.Hawa wanafanana sana na day trader huwa wanaingia na kutoka katika soko ndani ya siku husika

POSITION TRADER
Hawa huingia katika trade kwa siku kadhaa au week. Hii ni aina nzuri kwa wale ambao hawana mda wa kuangalia chart kila siku.

Hawa pia tunaambiwa ni traders ambao wanachukua profit sana ukizingatia wanakua kwenye market kwa mda mrefu hivo kuchukua faida ya week au mwezi. Hivyo aina hii ni kwa wale wenye mitaji mikubwa

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x