Jinsi Forex Trading Inavyofanya Kazi

Forex inafanyika kwa kulinganisha thamani za Sarafu Mbili kwa pamoja (Currency Pairs).


Kule sokoni unapoingia, ili uweze kununu na kuuza, utakuta bidhaa (currency) zimewekwa kwenye mafungu mafungu ya mbili mbili (pairs).

Mfano:
i)Euro na US Dollar pamoja,
ii) Paund (GBP) na USD pamoja,
iii) USD na Yen (JPY) pamoja,..nk. nk. nk


Zinavyopangwa, utazikuta hivi:
EUR/USD
USD/JPY
GBP/USD
USD/CAD

Chukua EUR/USD kwamfano;
Hiyo ya mwanzo (EUR) Inaitwa BASE currency, na hiyo ya pili, USD, unaitwa COUNTER Currency. Sasa, bei unazoziona kwenye grafu zikipanda na kushuka ni bei za Base Currency kwa kulinganishwa na Counter Currency. Chukulia hii;

EUR/USD = 1.25358

Maana yake, Euro 1 = 1.25358 USD. Kama unataka kununua EURO 1, utalipa1.25358 USD.

Bei za Euro sokoni, kwa kulinganishwa na USD, zinaweza kubadilika ndani ya sekunde! Sasa, faida zinapatikana kwa wewe KUNUNUA Currency moja, wakati bei iko chini na KUIUZA wakati bei inapopanda. As Simple as that. Sasa, ili kujua kwamba baada ya muda itapanda ili UNUNUE sasa hivi na uuze itakapopanda, au, kujua kwamba itashuka zaidi ya hapo ilipo ili, UUZE sasa hivi na UNUNUE itakapofika bei ya chini zaidi,…mchakato huo unaitwa MARKET ANALYSIS.

Forex Trading, hufanyika kwa “Kubonyeza tu” kitufe cha kuBUY au cha kuSELL. Basi. Hilo tu. Unakuwa umefanya TRADE na unakuwa umeingia kwenye trade na kusubiri matokeo. Lakini sasa, ili uweze kujua, unabonyeza kipi, muda gani, uTRADE kiasi gani ili upate faida gani, inabidi uwe unajua kufanya MARKET ANALYSIS mwenyewe au uwe na MTAALAMU unayemuamini akufanyie na akupe taarifa hiyo. Sasa, hiyo taarifa ndiyo inaitwa “Fx Signals” au “Trade Signals”..nk.

Faida au hasara kwenye Forex Trade zinapimwa kwa PIPS.

PIP ni kitu Gani? Kitefu chake ni “Percentage In Point”. Pip ni tofauti ya POINT MOJA katika bei ya Pair ya Currency tokea ulipoweka ORDER yako. Its a 1 point Price Movement ama kwenda juu au kuja chini.

Hii tofauti ya bei (Pip) inapimwa katika viwango vya Desimali. Currency Pairs nyingi (sio zote tafadhali) zinatumia SEHEMU NNE ZA DESIMALI. Utakuta kwenye Platform wanaandika SEHEMU TANO lakini ni ili kukusaidia wewe mfanyabiasha, ila zinazohesabika ni NNE.

Utaelewa vizuri kwenye mfano. Chukulia hiyo ya pale juu:

EUR/USD = 1.25358

Tunaangalia “Price Movement” katika sehemu ya 4 ya desimali. Ile ya tano inakupa tu sehemu ya Pip.

Chukulia hapo bei ibadilike ama kwenda juu au chini kama ifuatavyo:


EUR/USD = 1.25358
Bei Ikaenda Chini

EUR/USD = 1.25458
Bei Ikaenda Juu

Kutokea 1.25358 kwenda 1.25458 maana yake bei imepanda kwa pips 10.

Kutokea 1.25358 mpaka 1.25258 bei imeshuka kwa pips 10.

Swali, je kutoka 1.25258 mpaka 1.25200?

Jibu, imeshuka kwa pips 5.8 Sawa mpaka hapo?

Kwa hiyo, FAIDA na HASARA katika Forex zinapimwa kwa PIPS. Ukiwakuta watu wanaambiana, mimi leo nimepata, 30 USD, 50 Yen, 70 Paunds…unajua tu hawa sio professionals. Kule watu wanajisifia Pips sio Dola au Paundi au Yen. Utakuta mtaalam anasema, Mimi ninapata Average/Wastani wa 500Pips, au 700Pips au 1100Pips kwa wiki au kwa mwezi, nk. Sio Dola! Na mtaalamu anayependwa na wateja,..Anayeaminiwa kwamba anao uwezo wa Market Analysis mzuri ni yule anayejikusanyia PIPS nyingi mwisho wa siku.

Swali: Je, unaweza kupata PIPS kidogo na ukawa na faida KUBWA kuliko aliyepata PIPS nyingi kunizidi?

Jibu: Ndio. Inawezekana! Lakini, wooote, tutakujua kwamba huna PROFFESSIONALISM bali umeRISK sana na ungeweza ukapoteza hela nyingi sana pia! Sema tu bahati yako leo.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x