Jinsi Ya Kuchagua Forex Broker

Linapokuja suala la kuanza kufanya biashara hii ya forex , kuna vitu kadhaa ambavyo unatakiwa kuvizingatia kwanza.

Kitu cha kwanza nadhani ni kuchagua BROKER ambae atakufanya iwe rahisi kufanya biashara. Na katika kumchagua broker vitu vifuatavyo ni muhimu sana kuvizingatia:


LOW SPREADS.
Hii ni tofauti ya bei ya sarafu kutoka pointi inaponunuliwa mpaka pointi ya kuuza. Brokers wengi hawachukui commision hivyo hii spread ni sehemu ambayo huingiza pesa zao. Ukifuatilia kila broker utakuta wana tofautiana kiwango hiki cha spread, hivyo broker ambaye ana spread ndogo atakusaidia kukufanya uanze kupata faida mapema/haraka hivyo jitahidi kumtumia broker ambae anaoffer spread ndogo kabisa.

QUALITY OF THE INSTITUATION.
Brokers wengi huweka ushirikiano na bank mbalimbali au mashirika ya mikopo kulingana na kiasi kikubwa cha mtaji kinachohitajika. Pia broker lazima awe amesajiliwa na FUTURES COMMISION MERCANT(FCM) pia awe amepewa uhalali wa kufanya shughuli hio na COMMODITY FUTURES TRADING COMMISION(CFTC). Haya yote yanapatikana katika website za brokers au website za kampuni zao.


EXTENSIVE TOOLS AND RESEARCH
Forex brokers wanatoa vifaa vingi tofauti kwa ajili ya kukusaidia katika trade zako. Aina hizi tofauti huonesha vitu kama real-time charts,technical analysis tool,real-time news data hata pia baadhi ya msaada katika namna ya kutrade. Hivyo kabla hujamtumia broker jaribu kuomba platform yake kwa ajili ya majaribio ili ujue ni jinsi gani amekuwa bora.

A VARIETY OF LEVERAGE OPTIONS.
Leverage ni kitu cha msingi zaidi katika hii biashara ya FOREX. Hiki ni kiasi ambacho broker anakukopesha ili uweze kuingia katika trade. Mfano ukiwa na akaunti ya $100 unapopata leverage ya 500:1 hii inakusaidia kukupa uwezo wa kufanya trade ambazo zitaingiza mara tatu ya huo mtaji wako. Unachotakiwa kukumbuka low leverage ratio inamaanisha fursa ndogo ya magin call, lakini pia itakufanya ushindwe kufanya hata position zaidi ya tatu na kuendelea.


BROKER UNAYETAKIWA KUMUEPUKA.

Kama ilivyo kwa broker ambaye unahitaji kumpata/kumtumia pia kuna aina ya broker ambao unatakiwa kuwaepuka. Mfano broker ambaye amekuwa akisogeza mbele entry point unavokuwa umepress order yako. Inawezekana umepress order ya kubuy katika 1.23450 lakini unaona imefunguka katika 1.23420. Hii ni michezo ambayo huchezwa na baadhi ya brokers ili kujiongezea faida wao.

Kiujumla hakuna broker ambaye atakubali au kuandika hiki katika website yake kama anafanya hivi, bali kna njia kadhaa za kutambua aina hii ya broker.

Njia sahihi ya kugundua hili ni kuongea na wafanyabiashara wengine wa forex kujua broker husika anafanyaje. Hakuna orodha yoyote ya taasisi ambayo inaelezea aina hii ya udanganyifu hivyo kwa kujadili na wafanyabiashara wengine itakusaidia kutambua jambo hili. Waweza kumfuata mtu moja kwa moja au kutembelea majadiliano yanayokuwa yakifanyika online kufuatilia hili.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x