Terminology Za Forex Na Misamiati Yake

Ujue kwenye kila shuguli huwa kuna rugha ambayo huwa inatumiwa kwa kila aina ya shughuli. Ndio maana jinsi unavyoongea na rafiki zako ni tofauti na unavyoongea na baba au mama yako. So kwenye forex kuna rugha na maneno ambayo huwa yanatumiwa mara kwa mara na kama trader inabidi ufahamu haya maneno yana maana gani. Terminology Za Forex

BASE CURRENCY
Hiki ni kiini msingi katika kununua au kuuza katika forex. kama utabuy USD/JPY Hii ni kumaanisha unanunua dola ya kimarekani na wakati huohuo unauza yen ya kijapani.

Kwa maana nyingine Base currency in fedha unayoitumia wewe
Kwa mfano sisi Tanzania base currency yetu ni shillingsFelix

Kwenye Forex utatambua base currency kwa kuwa inakuwa ya kwanza kwenye pair mfano USD/JPY

Hapa USD ni base currency yako

QUOTE CURRENCY
Hii ni ile sarafu ya pili katika pair ya sarafu husika unapofanya trade. Mfano USD/JPY, JPY ndio quote currency.


LONG/BULLISH
Hii ni termonology ambayo unasikia watu wakiiongelea. kama imepatikana opportunity ya kulong/bullish hapa maana yake NUNUA. Bull ni aina za mnyama ambae anakula majani hivo candlestick zake nyingi zinakuwa zikiwakilishwa na rangi ya kijani. Huyu mnyama akitaka kukudhuru huinamisha kichwa chini na anakunyanyua kwa kukuchota kukupeleka juu. Hivyo katika Forex hapa inamaanisha soko linatoka chini linapanda juu.

SHORT/BEARISH
Kama imepatikana opportunity ya kushort/bearish hapa maana yake UZA.. Bear ni aina ya mnyama ambae anakula nyama, hivo candlestick yake huwakilishwa na rangi nyekundu. Huyu mnyama anavyokudhuru huruka juu kisha hukushusha chini. Hii katika forex inamaanisha soko linatoka juu kushuka chini.

Terminology Za Forex Na Misamiati Yake

PIP (PERCENTAGE IN POINT)
Hiki i kiasi cha thamani kinachocheza kulingana na mzunguko wa sarafu husika katika biashara. Huanza kuhesabiwa kutoka desimali ya nne katika pair mfano thamani ya USD/CHF ni 1.1379, thamani hii ikimove toka 1.13*79* mpaka 1.13*80* hapo inakuwa ni 1 pip
Isipokuwa kwa pair inazohusisha sarafu ya YEN nafasi za decimal zitakuwa tatu na sio nne kama pair nyingine. Mfano USD/JPY=1.137 hivo pip unaanza kuhesabu kwenye 7

TAKE PROFIT (TP)
Hili ni eneo ambalo utaamua kutoka nje ya soko baada ya faida. Eneo ambalo utaona faida uliyopata inakutosha au ni eneo ambali price inaweza kugeuka na kukuingizia hasara.
Unapoingia kwenye soko analysis zako zinakuonesha sarafu itapanda/kushuka mpaka eneo Fulani then baada ya hapo itageuka trends Ila haujui itachukua mda gani mpaka kufika katika hio price. Sasa huwezi kukaa kwenye screen yako mda wote kuisubiri hio point. Unachokifanya unaset kwamba price ikifika katika hilo eneo trade yake ijifunge automatically kisha ww ukirudi au ukimaliza mambo yako kama itakuwa ilifika katika hio point uje ukutane na profit yako. Hapo ndo panaitwa TAKE PROFIT.

STOP LOSS(SL)
Hili ni eneo ambalo utaamua kutoka nje kwa hasara either kwa kuona analysis yako ilikuw na makosa au unaamini upande wa hasara uliopo utaongezeka zaidi hivyo badala ya kupata hasara kubwa unaamua kuchukua hasara kidogo. Wanasema kama hutakubali hasara basi jiandae kupokea mama wa hasara kwa lazima.
Kwenye market ukishafanya analysis unaona kuna fursa ya kupanda kwa sarafu hivo unaamua kuinunua ikiwa chini ili ikifika juu uiuze na ile tofauti ya bei ulonunua na utakayokuja kuuza ndo inakuwa faida Na wewe uliingia sokoni kwa hio currency labda, Sasa baada ya kufanya hio analysis inatokea news mfano ya kushuka kwa ajira mfano marekani So kwa namna yoyote currency baada ya kupanda itashuka… Maana itakuwa weak.Sasa unakuta na wewe ulishaingia so unagundua itashuka sana hivo unaamua kutoka katika soko katika hasara ndogo ili usipate hasara zaidi kwani haujui hio currency itashuka mpaka wapi. Hio ndo inaitwa STOP LOSS

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x