Thamani Ya Pip Na Namna Pips Zinavyofanya Kazi

Nini Thamani ya PIP moja? Ili nijibu hili swali, kuna maelezo lazima nikupe. Ila kwa kifupi, thamani ya PIP moja inaweza kuwa ni 10 USD, au 1 USD, au 0.1 USD. Angalia:

Kumbuka, hii ni biashara kubwa sana. Kule kwenye soko la dunia, CURRENCY zinauzwa kwa jumla. Huwezi kwenda kununua eti Dola 1, au Paundi 5 au Euro 8. No. Unanunua kwenye mafungu! Huku kwenye forex kuna mafungu matatu tu maalum yanayouzwa:

a) 100,000 USD, au
b) 10,000 USD, au
c) 1,000 USD

Kwani hata Buteau de Change si wanauza kwa mafungu? Utakuta;

1 – 50 USD ina bei yake
51- 100USD ina bei yake
101- 1000USD ina bei yake
N.k. nk, nk..ndo ivo ivo kule.

Sasa,..

Wale waliosoma Science Sekondary mnikumbushe hii: S.I Unit maana yake nini tena? International Standard Unit? Nimesahau. Ila maana yake ni hii. Kipimo maalum kilichokubalika dunia nzima kupimia kitu mfano;
Urefu, S.I.Unit ni Meter
Ujazo, S.I.Unit ni Litre
Uzito, S.I.Unit ni Gram
N.k, n.k,…

Sasa kwenye Forex, kipimo kilichokubalika kupimia kiwango cha MAFUNGU ya kuuza na kununua Currency kinaitwa “Lot” Tumezoea kuita, “Standard Lot”.
Lot moja ukiigawa kwa KUMI utapata 1 Mini~Lot.
 Mini~Lot moja ukiigawa kwa KUMI (au Standard Lot moja ukiigawa kwa MIA) unapata 1 Micro~Lot.

Angalia sasa;

1 Std Lot = 100,000 USD,
1 Mini~Lot = 10,000 USD
1 Micro~Lot = 1,000 USD
Nenda kinyumenyume, utaona kwamba:

1lot = 10 mini~lots = 100 micro~lots

Au kwa namna nyingine;

1Micro~lot = 0.1 Mini~lot = 0.01lot.

Sasa, unapokwenda KUPLACE ORDER ya kuBUY au kuSELL kuna sehemu utaulizwa ujaze SIZE ya ORDER yako. Utajaza 1Lot kwa maana ya unanunua au kuuza 100,000USD au utajaza 0.1lot kwa maana ya unauza au kununua 10,000USD au utajaza 0.01lots kwa maana ya unauza au kununua 1,000 USD.

Sasa twende kwenye thamani ya PIP.

Endapo ULIUZA au KUNUNUA “1 Standard Lot”, kila PIP moja unayoipata sokoni kama faida, ni sawasawa na 10 USD. Maana yake, kwa 100,000 USD ulizoTRADE, umepata faida ya 1PIP au 10 USD.
Kama uliTRADE 1minilot, 1PIP ni sawa na 1 USD na kama uliTRADE 1 microlot, PIP moja ni sawa na 0.1 USD.

Umenielewa mpaka hapo? Ngoja nikusisitize yafuatayo kama NB.

Note1: Si kila Currency Pair PIP yake inapimwa kwa 4decimal places. Kuna baadhi sio, mfano Currency Pairs ambazo zina Japaneese Yen ndani yake kama EUR/JPY au USD/JPY na zingine, PIP yake moja inahesabiwa katika sehemu MBILI za Desimali. Ukishakuwa sokoni utazizoea tu usiogope. Utazijua zote.

Pips ni nini

Note 2: Sio kila 1PIP ni sawa na 10 USD kwa 1lot. Kuna tofauti zake pia. Baadhi ya currency pairs, 1lot zao, 1PIP utakuta ni 8USD, 11USD au hata 7USD. Inategemea. Ile ya 1Pip = 10 USD ni Standard. Utazielewa pia ukishaingia sokoni. Ila mpaka hapa, unaweza kuelewa kwamba, aliyepata 25pips za 1lot za:
i) EUR/USD,
ii) EUR/JPY, na
iii) GBP/USD
wanatofautiana kwenye hela kwa sababu thamani ua 1PIP kwao zinatofautiana. Ila tofauti zao si kubwa saaana. Zoote, zinakaribi pale pale kwenye Kwa 1std lot, 1Pip = 10 USD.

Hivi Kweli, kuna Retail Trader ataweza kununua 1lot, au 1minilot, au hata 1microlot (kiasi cha chini kabisa cha order moja ambacho ni 1000usd = 2.4mil Tzs) na akasavaivu kwenye hii biashara kweli. Huko si ni kubaguana? Wataifanya wenye nacho tu, si ndiyo?

Hapo sasa, ashukuriwe Mungu kuna Mtukati anaitwa Broker. Ndiye anayetuwezesha mimi na wewe tushiriki Forex. Vingenevyo, ingebaki kuwa ni biashara ya Mabenki, Serikali, Taasisi kubwa kubwa za Kifedha ma Matycoon wakubwa.

Kazi kubwa ya Broker ni kukukopesha hela zake ili uzifanyie biashara ya Forex. Atakuambia kwamfano; ukifungua account ya mtandaoni kwangu, uka~deposite hela, kwa kila Dola 1 utakayo~deposite, nitakukopesha Dola 100 au, 200, au 500 au wengine mpaka 1000! Hicho kitendo kinaitwa “Leverage”. Wanaandika hivi:

Leverage:
1:50 (kwa kila dola 1 uyakayoweka kwangu, nakukopeaha 50), au
1:100 (weka 1, kopa 100), au
1:500 (weka 1 kopa 500) n.k, n.k

Kwamfano sasa, ukiweka USD 100 kwenye account yenye Leverage ya 1:500 maana yake ni nini?

Kwa kila dola 1 uliyo~deposite anakukopesha dola 500. Kwa hiyo, jumla utakuwa na dola 100 x 500 = 50,000. Hiyo inaitwa “Purchasing Power”. Hapo maana yake ni kwamba unauwezo sasa wa kununua au kuuza USD 50,000 ambayo ni sawa na 0.5 lot size, tofauti na awali ambapo ungetegemea 100$, usingeweza kuuza au kununua chochote (hata order ndooogo kabisa ambayo ni Micro~Lot = 1000usd).

Brokers wanakuchaji wewe comission wakati wowote unapoTRADE, ndipo kipato chao kilipo.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x