Jinsi Ya Kutumia Forex

Kuna watu wengi wanajiuliza maswali mengi, juu ya jinsi ya kutrade forex, jinsi ya kufanya biashara ya forex, namna ya kufanya forex, namna ya kufanya biashara ya forex, na jinsi ya kutumia forex, hii yote ni wanataka kujua biashara ya forex inakuwaje mtu anapata faida, na natumaini ndio maana uko hapa unasoma hii post ili uelewe namna ya kufanya biashara ya forex so ngoja nikupe jibu.

Kuna Hatua Sita ambazo unazipitia ukiwa unataka kutrade forex

  • Kwanza unachagua pair ambayo unataka kutrade mfano EURUSD au USDJPY.
  • Pili unafanya market analysis na kusoma chart kwenye hiyo pair uliyoichagua na kujaribu kutafuta ni uelekeo upi ambayo bei ya hiyo pair itaelekea ili uweze kutengeneza faida.
  • Ukishafanya analysis na ukagundua kuwa bei ya hiyo pair EURUSD itaenda juu basi unaenda kulia juu kwenye chart na ku-click BUY. Kama umefanya analysis na ukaona bei itashuka chini una-click SELL.
  • Weka Stop loss levels na Take profit levels. Stop loss ni sehemu ambapo kama bei ikienda tofauti na ulivyopanga basi stop loss itazuia usipata hasara kubwa. Take profit ni sehemu ambayo unataka bei ikifika trade itajifunga na utakuwa umetengeneza faida.
  • Fatilia trade yako uliyoingia kama inaenda sawa au haiendi sawa
  • Funga trade yako. Kama ulikuwa sahihi utakuwa umetengeneza faida, na kama ulikosea basi utakuwa umepata hasara.

Hatua ni sita tu ambazo zinatumia kutrade forex na zinaonekana rahisi ila ngoja nikwambie kitu

Jinsi ya kutrade forex kwanza unachotakiwa kujua ni kwamba kuna kitu huwa tunaita market analysis. Hii ni process ambayo wewe kama forex trader unatakiwa kujua jinsi ya kufanya market analysis Ukishajua namna ya kufanya market analysis au uchambuzi wa soko ndio sasa utaweza kutrade na kutengeneza faida kila siku.

Unafanyaje Market Analysis?

So nina uhakika swali ulilonalo sa hivi ni unafanyaje market analysis?

Market analysis au uchambuzi wa soko unafanyika kwa kusoma kitu tunaita Forex charts kama hiyo picha hapo chini.

Namna ya kufanya biashara ya forex

Ukijua namna ya kusoma forex chart na kuelewa mwenendo wa soko la forex unavyoenda ndio itakusababishia wewe kuwa forex trader mzuri na kuwa unatengeneza faida kila siku iendayo kwa mungu. Ishu inakuja kwenye namna ya kusoma forex charts.

Namna Ya Kusoma Charts

Sasa hapa ndio Mabalaa yanapoanza. Kujua namna ya kusoma charts au kufanya markets analysis ndio kazi kubwa ilipo. Hii ni kama vile unatakiwa kwenda chuo ujifunze namna ya kusoma charts na kufanya market analysis. Mimi imenichukua takribani miaka mitatu mpaka minne kuelewa namna ya kusoma charts ila hii ni kwa sababu nilikuwa na kazi zingine, ila kama ukiweka mda na ukajifunza ndani ya miezi sita mpaka mwaka mmoja unaweza kuanza kuelewa namna ya kusoma charts na kufanya analysis.

So Namna ya kusoma charts inabidi ujifunze mwenyewe na kufanya mazoezi kwenye demo account. Kama ulivyosoma kwenye post, Jinsi Ya Kuanza Biashara Ya Forex utagundua kuwa nilisema unachotakiwa ni kufungua demo account kwa broker na kuanza kutrade na kufanya mazoezi. Mazoezi, Mazoezi Mazoezi ndio yatakayokufanya uwe strong kwenye soko la forex na ukifanya mazoezi na kuweka mda wako kujifunza strategies za namna ya kutrade forex utakuwa mbali.

Trading Strategies Ndio Nini.

Kwenye soko la forex kuna kitu kinaitwa trading strategy na hizi ni njia mbalimbali ambazo zinatumika kutrade forex. Kuna strategies nyingi sana kwenye soko la forex na kama unataka kuhakikisha we nenda youtube na u-search “Forex Trading Strategy” utaona strategy zitakavyomiminika mbele yako, na kazi yako inakuwa ni kuangalia hizo videos uzielewe na urudi kwenye account yako demo na kufanya mazoezi.

Sehemu Za Kujifunza Namna Ya Kutrade Forex

Babypips.com


ili ujue namna ya kusoma charts na kufanya market analysis na namna ya kutrade kuna hii website babypips ni nzuri sana kwa kuanza wana content nzuri sana zinazohusu namna ya kutrae na mambo yote yanayohusu forex trading, unaweza kui-check it out.

Youtube

Youtube ni sehemu ambayo unaweza kujifunza strategy nyingi na vitu vingi vinavyohusu forex trading. Nimefurahi sana hata hapa Tanzania kuna channel nyingi sa hivi ambazo zinaongelea forex trading which is really good so we nenda youtube search forex tanzania kuna content nyingi utakutana nazo.

Watu wengi wanasema youtube videos hazifundishi vizuri na kuna wakati unahitaji kuwa na mentor kabisa ukae nae pembeni akuelekeze, Well kama ni hivyo kwanza kuna webnairs.

Jinsi ya kutrade Forex

Webnairs

Webnairs ni mikutano ambayo ipo online natumaini utakuwa unaijua so ukiona watu wanatagaza webnair inayohusu forex trading basi we andaa bundle la internet la kutosha ujiunge kwenye mkutano na ukafudishwe wakati upo hapo hapo sebuleni kwako au chumbani kwako.

Seminars

Seminar nyingi sa hivi zipo hapa Tanzania na zinazidi kuja na kuja, baadhi ni bure na zingine ni za kulipia so ni wewe kuhakikisha unaenda kwenye hizo seminars kama ukiwa na mda maana kila seminar wanafundisha tofauti so unaweza kujifunza kitu kipya kwenye kila seminar inayohusu forex trading.

Mentors.

Mwisho kabisa kuna mentors ambao wao wanatoa haya mafunzo kwa bei zao na gharama zao. So mentors wanaweza kutoa mafunzo kwa mfumo wa seminar au webnairs au one on one training uka kaa nae hapo akakufundisha mpaka ukaelewa. So ni wewe tu kutafuta mentor mzuri akufundishe namna ya kutrade mpaka uelewe.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x