Njia nzuri ya kujifunza kutrade Forex

Je! Unatamani kujifunza biashara ya Forex, na wakati mwingine unatapata wakati mgumu hata kujaribu kutrade? Basi ni wakati wa kufahamu zaidi mambo ya Forex –

Kwanza, somo la historia: Forex, au soko la fedha za kigeni, linataka kuwa kubwa kwa uzalishaji mkubwa wa pesa, mashirika, benki kuu, na watu wenye pesa sana. Lakini vitu vingi vimetokea hasa baada ya internet kuja kila kona ya dunia imerahisisha kila mtu aweze kujihusisha na maswala ya forex kwa kutumia brokers.

Njia nzuri ya kujifunza kutrade Forex

Jifunze kwanza vitu Basic vinavyohusu forex.

Ni muhimu kuelewa mambo ya mwanzo yanayohusu forex kwa sababu ukianza kusoma vitu vikubwa kuna baadhi ya vitu utamiss na kujikuta unasoma vitu ambavyo ni vizuri ila bado una lose trades like crazy. Sasa hapa watu wengi sana hata mimi wakati naaanza huwa tuna waza Get Rich Quick. Yaan tunafikiri forex. Trading ni very simple so kuanza kujifunza vitu basic tunaona kama ni kupoteza mda. Me nakumbuka nilikuwa naambiwa price action ndio strategy nzuri but me sikutaka kusoma kwa sababu nilikuwa naona indicators na systems ndio nzuri so nilichokipata ni kuunguza accounts like crazy.

So ili uwe trader mzuri unatakiwa uanze kujifunza vitu basic kwa maana ya kuelewa forex ni nini, inafanyikaje, risk management na vitu vingine kabisa kabla hata hujaweka trade hata moja.

Jifunze Risk management

Risk management is the game in forex my friend. Nakumbuka wakati naanza kutrade risk management niliona kama inanirudisha nyuma hadi sometimes nikawa siweki stop loss. Dont do that men,…..dont do it

Ni muhimu sana na ni lazima ujifunze na uwe nondo sana kwenye swala la risk management kwa sababu katika hali ya kawaida unatakiwa kulinda account yako wakati unatrade. Kama ushawahi sikia watu wanasema unaweza kuwa na strategy nzuri but kama hauko vizuri kwenye risk management, lazima uingie Chakaaaa over and over. Kutrade bila risk management ni kama kuendesha gari wakati hujui kuendesha, lazima tukuokote chini ya mto.😁

Anza kutrade na Pair chache

Wakati naanza kutrade nilikuwa natrade almost pair 12 kwa siku na tena natumia 1min chart.. Thats insane kabisa na nilikuwa newbie. Hii ilinifanya nipate wakati mgumu kufatilia pair gani ni nzuri kutrade na mda fani ni mzuri kutrade hiyo pair.

So kwa kuanza ni vema ukaanza na pair atleast 3-6 pairs ambazo utakuwa unazifatilia kwa karibu. Sa hivi mimi naangalia 8 pairs na hii ni kwasababu nimeona kuangalia pair nyingi inachanganya sana so ukifocuc kwa kuwa na pair chache ni rahisi kuzifatilia na kujifunza wapi umekosea.

Trade Demo Account

Demo account a.k.a Demonstration Account. Hii ni account ambayo kila newbie anatakiwa kuanza nayo, kwa sababu ni account ambayo itakusaidia kutrade kwa kutumia real market prices na utakuwa unatrade kwa hela ambazo sio real. Demo account inakusaidia kufanya mazoezi na kuelewa zaidi jinsi watu wanavyotrade forex.

So unatakiwa kufungua demo account kwa broker ili ujifunze kutrade taratibu kabla hujadeposit hela zako.

Kitu muhimu wakati unafungua account ni kwamba unatakiwa kufungua demo account ambayo ina balance ambayo utakuja kuitumia ukianza kutrade in real account. Mfano kama wewe umeshapanga kudeposit 100usd basi wakati unafanya mazoezi kwenye demo, anza na balance ya $100 na sio ya $1000 au $5000, kwa sababu ukianza na account kubwa kuliko amount utakayodeposit itakufanya uumguze account kwa sababu kwenye demo ulikuwa unamake 50usd profits af kwenye real baabda ya kudeposit hako ka mia utakuwa unamake 2, 5, 10, so hii itasababisha uanza kutrade against the plan, na kutumia lot size kubwa kuliko uwezo wako na mwisho Unaunguza account. So ni muhimu sana hii kitu na imenisaidia sana.

Jaribu kufanya Weekly Analysis

Weekly analysis huwa zinafanywa on weekend. Wengine wanafanya jumamosi wengine jumapili, mimi huwa nafanya jumapili. Weekly analysis ni nini ? Hiki ni kile kitendo cha kusoma charts na kujaribu kuangalia kama kuna set up zinazoweza kutokea week ijayo. Yaani ni kama unajiandaa na week ijayo. So badala ya kusubiri mpaka market ifunguliwe ndio uanze kuangalia chart, we on weekend jumapili au jumamosi kaa kwenye chart na uangalie ni aina gani za movement zinaweza kutokea market itakapofunguliwa, na wakati mwingine hii inakusaidia kujua kama kweli unajua kulisoma soko la forex.

Tengeneza Straregy.

Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua kuhusu strategies ni kwamba kila mtu anatumia strategy ambayo YEYE mwenyewe ameona inamfaa. Kwa hiyo wakati unatafuta strategy ya kutumia kutrade utakutana na watu wengi wanafundisha strategy mbalimbali na wewe kazi yako ni kuchagua strategy ambayo itakufaa, Kwa sababu kuna mtu akitrade na indicators ana win zaidi kuliko akitrade price action strategy.

Traders wengi wanalose trades kwa sababu wanabadilisha badilisha strategy kila mara na wanabadilisha bila kujua kwa nini wamebadilisha, katika hali ya kawaida unatakiwa kutrade na kutengeneza strategy yako kwa muda usiopungua miezi mitatu mpaka sita, hii ni kwa sababu unahitaji mda mwingi wa kufanya majaribio ya strategy yako ili uwe vizuri ukienda live. Atleast ukipata strategy ya asilimia atleast 60-70 percent ni nzuri zaidi.

Anza na Account Ndogo Kwenye Real Account

Unapoanza kutrade forex kwenye real account ni vema ukaanza na ammount ndogo kwanza. Hii ni kwa sababu wakati unatrade kwenye demo ulikuwa unajua ni demo tu na hamna kitu unachopoteza ila sasa ukishaweka hela yako tu na trade ikaenda against emotions zinakuja unaanza kupanic, kwa nini unapanic??¿?? Kwa sababu unajua utalose hela, so ikitokea umelose basi upoteze kidogo ndio maana ni vema ukaanza ana amount ndogo.

Soooooo!!!

Soo hapo nimekuelezea namna ya kujifunza kutrade ila kitu ambacho sijasema ni wapi unaweza kupata information za kujifunza, well kwanza kabisa kama kawaida utaanzia google search material yapo mwengi na vile vile youtube kuna channel nyingi zinaelezea za kiswahili na kiingereza na mie nitakuwa naweka zangu taratibu. Ishu kama una swali nitafute iwe telegram au insta then nitaona namna ya kukusaidia.

Wakati unatest strategy, skills, emotions au mihemko. Forex ni rahisi kama unajua unachokitafuta, so make your plan and trade your plan. Good Luck.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x