Trading Strategy Ni Nini Hasa?

Whats up! whats up! guys how are you doing hope your Goodei…..

So what the hell is a trading strategy? A.k.A Trading strategy ni nini?

Trading strategy ni kama njia ambayo utakayotumia wakati unatrade forex. Me huwa napenda kutumia mfano wa kuwinda wanyama porini. Ujue kutrade forex ni kama hunting au kuwinda kwa sababu wewe unavoingia kwenye trade ni kama umeingia kwenye msitu unaenda kuwinda, sasa ishu iliyopo ni kwamba, market maker a.k.a the big banks nao wanakuwinda na wanatafuta stop loss yako ilipo ili waibamize ufe na uunguze account, wakati wewe unataka kupata ka nyama kidogo tu af ulale mbele kambla stop loss yako haijakutwa. So ukiangalia ni kama vile tunawindana flan hivi kwa sababu sis retail traders ni wadogo sana na tunajaribu kupata kipande kidogo cha nyama kwenye hili soko la forex.

So kwa kutumia mfano huo strategy ni kama silaha ambayo utaitumia kwenda kuwinda unapoingia porini. Kama kwenye kuwinda kuna kuwinda kwa kisu, panga, manati, bastora, Gobore, au kama wazee wa ngwasuma unatumia mjegejo mashine gun grrrrrrrrrrrr,……..Huku kwenye forex pia kuna njia nyingi za kutrade au strategy nyingi za kutrade. Kuna kutrade kwa kutumia signals
Indicators
Robots
Price action
Pattens
Na strategy nyingine kibao yaani strategy zipo nyingi kama yoteee.

Sasa basi kabla hujaanza kuchanganya mafile nataka nikuonyeshe kitu kimoja rahisi saana ambacho nimegundua wakati natrade.

Trading Strategy ili iitwe Strategy inatakiwa iwe na vitu Vitatu Tu. Hakuna siasa wala nini ni vitu vitatu tu inatakiwa kuwa navyo.

1. Conditions
2. Entry Reasons (Sababu za kuingia kwenye trade)
3.Exit

1. Conditions

Conditions hii ni hali ambayo market inatakiwa iwe ili wewe uweze kuanza kutafuta trading opportunities au kuanze kutrade. Yaani ni ile hali ambayo unasubiri markert iwe kwenye hali flan ili wewe uingie kwenye trade and crush it. Kama hujaelewa rudi kwenye mfano wa Porini hapa. Mfano kama unamuwinda simba conditions zako ni kwamba utasubiri mpaka simba alale ndio uweze kumvamia na kujaribu kumuua, so kwenye market unasubiri market iwe kwenye hali flab au mazingira flani ili wewe ndio uweze kuingia kwenye trade. Au kama unataka kumuibia mtu conditions zako si utasubiri mtu alale ndio ukamuibie si ndio eh?? Hope utakuwa umeelewa kama bado check hii video hapa utaelewa tu….lazima uelewe.

trading strategy

2. Entry

Ukishapata na kujua conditions zako

Kinachofata ni entry point hii inamaana, unatakiwa kujua sasa ni kitu gani utaangalia ambacho kitakufanya wewe uingie kwenye trade either sell au buy. Mara nyingi hapa huwa ndio tunatumia price action au candlestick patterns ambazo huwa zitakupa sababu ya wewe kuingia kwenye trade. So ni vizuri ujue kila kitu kuhusu price action and candlestick patterns.

3. Exit

Exit plan hapa unatakiwa kujua baada ya kuingia unategemea take profit target itakuwa wapi. Hii ni mapema hata kabla hujaingia kwenye trade unatakiwa kuwa tayari ushaijua. Sasa utakuwa unajiuliza mbona sijaongelea swala la stop loss. Well hii Mara nyingi huwa inategemea na balance yako na wewe mwenyewe kujipangia upo tayari kurisk sh ngapi kwa kila trade. But kisheria unashauriwa urisk asilimia 1-2 kwa kila trade, kwa mfano Mimi huwa narisk asilimia moja tu kwa kila trade na nakushauri urisk asilimia moja tu kwa kila trade, kwa sababu ni rahisi kumanage kama ukipata loss tatu mfululizo. Check this out, kama ukirisk asilimia mbili kwa kila trade na trade tatu za mwano ukapata loss hapo unakuwa umelose 6% percent ya aaccount yako, ila kama ungekuwa umerisk asilimia 1% kwa kila trade ungekuwa umelose 3% percent ya account yako, see how easy and simple? Ni simple sana hii hesabu so ushauri risk 1% kwa kila trade no matter what, ukishindwa basi mwisho 2% percent.

Kwa Hiyo!
Kwa hiyo I hope utakuwa ushajua trading Strategy ni nini na kwa ufupi tena hii ni njia ambayo unaitumia wakati unatrade na kuna strategy nyingi sana kiasi kwamba unaweza ukachanganyikiwa usipoangalia, kwa sababu kama usipotulia na kujaribu stratetegy moja baada ya nyingine ndio utakuwa na ile kitu tunaita information overload. So ushauri tu, fanya mazoezi strategy moja baada ya nyingine, usichanganye kwa sababu ukizichangaya utapata wakati mgumu kujua uzuri na ubaya wa strategy flan.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
gideon
gideon
11 months ago

ufafanuzi wako haueleweki mkuu

erekcjacompl
8 months ago

I think this is among the most vital info for me. And i am glad reading your article. But wanna remark on some general things, The site style is perfect, the articles is really excellent : D. Good job, cheers

error: Content is protected !!
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x