Unaipataje Trading Strategy?

Simple tu,..

Practice, practice practice. A.K.A fanya mazoezi ya hatari.

Nakumbuka wakati me naanza kutrade mwaka 2015 moja kwa moja nilianza kutrade kwa kutumia indicators, kama RSI,bollinger bands, Macd, na sytems zingine zingine nikanunua yaani nimetumia kila aina ya systems. Muda huo wote unakuta wiki hii natrade kwa indicator hii then week ijayo naanza kutumia nyingine, then weekend naona tangazo la system flan nainunua nikifiri nimepata system ya kuwa tajiri na matokeo yake hakuna kitu. Ila nakumbuka kuna mda nilitrade kwa kutumia RSI kwa mda wa miezi miwili ndio nikajiambia hiyo ni strategy yangu. Mda huo woote nilikuwa naona watu wanasema ili uwin kwenye forex jifunze kusoma price action, supoort and resistance, ila me nilikuwa mbishi nataka easy systems na nimepoteza mda mwingi kutafuta hizo systems mpaka nikaja kugundua kuwa ni bora nianze kusoma price action.

Nikasoma price action nikafanya mazoezi suport and resistance, na kusoma vitabu vya kutosha rudi demo fanya mazoezi, humo humo ndio nikagundua patterns, nikagundua trend line strategy na mambo mengi mabyo mpaka sasa bado nayatumia na bado naendelea kujifunza kwa sababu as humans we got to be ForeverNewbies Ha! .

So namna ya kupata strategy yako ni wewe kufanya mazoezi na kujaribu kila strategy mpaka upate strategy ambayo unaona unapenda kuitumia wewe mwenyewe, na uko na amani kuitumia.

unaipataje trading strategy

Kitu ambacho traders wengi tunachanganya ni kwamba kila mtu ana style yake ya kutrade na ana make profit. Me naweza kutrade kwa kutumia price action tu ila wewe unaweza kutumia indicators kibao hapo hadi candlestic hazionekani bado una make profit. So cha muhimu mtu akikufundisha strategy namna ya kutrade ni wewe kufanya maamuzi je unaipenda au la.

Ngoja nikurahisishie kazi kuna aina nyingi ya strategy so ni wewe kuanza kuchagua ipi inakufaa

Indicators Strategy
Patterns Strategy
Support and Resistance Strategy
Supply and Demand Strategy
Price action Strategy
Trendlines Strategy

Hizo ni baadhi ya strategy maaarufu ambazo kama trader unatakiwa kuzijua na kuchagua ipi ambayo unaipenda. Mimi sa hivi natumia almost zote ila sana sana natumia patterns, supports and resistance, na trend lines, bila kusahau Price action a.k.a candle stick patterns.

Soooooooo!

Trading strategy kwa kifupi ni njia ambayo utaitumia kutrade kwenye soko la forex na hii njia ndio itakayokufanya utengeneze profit au upate loss kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha unaielewa strategy yako vizuri kabla hujaanza kutrade na real money.

Good luck and welcome to the game……šŸ˜Ž

Time yako sasa niambie unapata shida wapi kwenye kutafuta strategy yako?

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x