Ukweli Kuhusu Kutrade Kwa Kutumia Indicators. Je Zinafanya Kazi?

Nakumbuka wakati naanza kutrade nilianza kutrade kwa kutumia indicator inayoitwa RSI na Bollinger Bands indicators. Yaaani ulikuwa huniambii kitu Na nakumbuka nilitengeneza some profits na nikawithdraw some na nikalose a lot. So indicators je Zinafanya kaziii au zinatuunguzia account zetu?

Jibu: Ndio indicators zinafanya kazi na zina leta faida KAMA…….Ukizitumia na strategy zingine vile vile kama unajua namna ya kuzitumia vizuri.

Ngoja nikupe maelezo ili uelewe vizuri. Wakati naanza kutrade nilikuwa natrade na RSI ambapo Mimi nilikuwa naangalia tu price ikiwa chini ya 30 na buy na ikiwa juu ya 70 na sell. Hivyo nilikuwa siangalii maswala ya trend, wala support and resistance wala cha price action. Me condition yangu ilikuwa moja tu price ikiwa chini ya 30 na buy na ikiwa juu ya 70 na sell. Unakuja kilichotokea nini? Nilikuwa napata loss zaidi kuliko wins, kwa Nini?…..kwa sababu nilikuwa naangalia kitu kimoja tu nilikuwa nategemea indicator peke yake kunipa sababu ya kuingia kwenye trade na ndio maana market ipo kwenye trend kali ya juu na RSI ipo juu ya 70 naingia sell then napata loss kwa sababu market inatrend kali ya uptrend na mie nilikuwa siangalii hiyo ndio maana nilikuwa naunguza account day in day out.

Kama Unajua Namna ya Kuzitumia Indicators Utapata Profits.

Kuna swala la kujua namna indicator inavyotumika. Kila indicator ina namna yake inavyotakiwa kutumika na set up zake na period zake kwa hiyo Kama trader yaani unatakiwa kujua namna indicator inavyotumika ili uweze kuchanganya na indicators zingine au strategy zingine, kwa sababu hutokuwa unatumia indicator moja kwa hiyo Ni vema kujua matumizi ya indicator flan yakoje.

Baada ya kufahamu namna indicator inavyotumika kitu kinachofata ni kuangalia sasa namna utakavyoichanganya hiyo indicator na strategy zingine.

Hapa Namaanisha Nini Sasa?

Kitu nilichojifunza na nilichofundishwa na YouTube na mentor wa bure ni kwamba….. indicators haitakiwi kutrade kwa kutumia indicator peke yake, badala yake indicator inatumika Kama njia nyingine ya kukuongezea sababu ya kuingia kwenye trade. Kwa kizungu tunasema tumia indicators Kama confirmation za set up flan ila sio kama signals.

Ngoja nitoe mfano, ila Kama hutaelewa angalia video hapa au chini nimeelezea vizuri.

Mfano unatrade support and resistance strategy na price imefika kenye support zone so wewe cha kufanya unaamua kuweka RSI ili uone kama price iko juu ya 70 na ukiangalia unakuta kweli ipo juu ya 70 so hapo unakuwa na confidence ya kuingia kwenye hiyo trade kwa sababu Kwanza price ipo kwenye support area na pili RSI ipo overbought huu ya 70. Huko ndio kuchanganya indicators na trading strategy.

Kutrade Kwa Kutumia Indicators

Kama unatumia moving avarage indicator kuna namna ya kuchanganya na strategy ambapo mara nyingi inatumika wakati unatrade kwa kufata trend, ambapo price ikienda chini ikarudi kugusa Moving Avarage unaingia tena sell kwa matumaini kwamba price itaendelea kushuka chini. Nimeelezea vizuri Sana kwenye video hapo chini au Click Hapa, vema ukaangalia taratibu ili uelewe vizuri.

Tip:>

Top three 3 Indicators ambazo zinatumika Sana na almost asilimia 80% ya traders duniani Ni

Moving Avarage

Relative Streangth Indicator RSI

MACD

So ili usipoteze Mda wako kutafuta indicators zingine ni vema ukaanza kujifunza kutumia hizi indicators 3 baada ya kuzielewa ndio uanze kuangalia indicators zingine. Got it!?

Soooooooo ¡!!¡!¡!¡

Kwa uzoefu wangu nimeshatumia indicator nyingi sana na systems kibao na kweli kama mentor’s wanavyosema indicators zinafanya kazi ukizichanya na strategy zingine na hii ni kweli na nimeshajaribu na nikagundua ni kweli na mpaka sasa nachanganya indicators na strategy zangu sometimes. Ukitrade kwa kutegemea indicator peke yake ndio mabalaa utayapata. Me Sana Sana natumia moving average na RSI ndio naendelea nazo mpaka leo na zinanisaidia Sana wakati nataka kuingia kwenye trade.

So tumia indicators Kama confirmation ya set up na vile vile bila kusahau price action, ukifanya hivyo lazima broker akuweke kwenye black list maana utakuwa unacrush the markets like Crazy……😎

Kumbuka….

Indicators Sio Signal Providers…..Zinakusaidia Tu Wakati Unapofanya Market Analysis.

Tell me Sasa we unatumiaje indicators je zinakusaidia au zinakuchanganya kabisa?

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
BrianMiz
1 year ago

Keep up the outstanding work !! Lovin’ it!

error: Content is protected !!
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x