Kwanini Inabidi Uanze Kujifunza Kutrade Forex 2020?

Kwanini unatakiwa kuanza kujifunza kutrade forex 2020

Kwanza kabisa kabla sijaanza kuongea maneno mengi, kwa mfano ukianza kutrade forex January 2020, na ukawa serious kabisa, ukifika mwezi wa 11 unaweza kuanza kutrade in Live Account, ila hata mwezi wa sita unaweza kuanza kutrade live kama wewe ni muelewa wa mabo haraka.

So the sooner the better. 

Alright whats up whats up guys how are you doing today hope your Greeeeeat!

Forex trading ni njia moja wapo ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza na kuweza kuanza kupata hela au pesa au money kwa kutrade forex tu. Yaaani ukijua kutrade forex unaweza ukawa unatengeneza pesa huku uko nyumbani bila hata kutoka nje. 

So kwanini inabidi uanze kutrade forex. 

  1. Ni njia ya kujiingizia kipato. 

Forex trading ni njia moja wapo ya kujiingiziq kipato kwa hiyo unatakiwa  kama unaweza na uko tayari inabidi uanze kujifunza kutrade forex kwa sababu ukiweza kutrade utakuwa umejiongezea njia nyingine ya kipato. Ukifanya trading forex kama biashara zingine lazima utatoka, ila ukifanya forex kama mchezo wa kubet, utaona forex kama gambling na utaichukia kabisa. So please wakati unaanza kujifunza kutrade forex please akilini kwako jua kuwa unaanza kujifunza namna ya kufanya hii biashara na kutengeneza faida kuliko hasara.

2. Sio Gharama Kuanza Kutrade

Ukitaka kuanza kutrade forex na hela za kweli au real money baada ya demo acccount, unaweza kuanza kutrade kwa mtaji wa shilingi elf hamsini au hata elfu ishirini na tano. Kwa hiyo hauhitaji kuwa na pesa nyingi ili uanze kutrade forex. Japo ukianza kutrade na hela kidogo kama elf hamisini na faida yake itakuwa ndogo, ndio maana me huwa nashauri ni bora uanze na angalau laki mbili na nusu au $100 usd, ukiwa na hela sana angalau anza na $250 usd kama laki tano.

3. Unaweza Kutrade Kwa Kutumia Demo Account. 

Uzuri wa forex trading au biashara ya forex ni kwamba hata kama hujui kutrade unaweza kuanza kutrade kwa kutumia demo account. Demo Account au Demonstration Account ni account ambayo ina kuwa na hela ambazo sio za kweli, ambapo huwezi withdraw zenyewe zinakuwepo tu ili ufanyie mazoezi. Kwa hiyo demo account ni account ya kufanyia mazoezi na kila broker anakuwa nayo. So ukitaka kuanza kutrade forex hii ndio account ambayo utatakiwa kuifungua na kuanza kufanya mazoezi na kujua forex inakuwaje na inafanyaje kazi.

unaipataje trading strategy
Forex Trading Ni Kama Biashara Zingine…. Kuna Hasara na Faida

Wewe kama hujui unaweza kuanza kutrade forex kwanza kwenye demo account ambayo ndio utakuwa unafanya mazoezi wakati unatafuta strategy yako baada ya kuwa umepata strategy yako ndio unafungua real account ambayo sasa unadeposit hela zako kutoka bank na ukipata faida unawithdraw na kwenda kununua Kitoweo. You know make money, spend money

4. Unachohitaji Ni Computer Na Internet. 

Ukitaka kutrade forex wala hamna mbwembwe, hakuna kusajili, hakuna kujaza form, wala hakuna kukodisha chumba. wewe unachohitaji ni computer na internet, off-course na umeme utahitajika so unaweza kuongezea na hiyo, ila ni wewe na computer yako tu ndio utakuwa mnahusika na hii ni nzuri kwa sababu hakuna udalali wala kuongea na mtu ni wewe na computer yako. Utahitaji kuongea na mtu pale utakapokuwa unataka mafunzo.

Kwahiyo??

Kwa hiyo mimi nataka uanze kujifunza kutrade forex mwaka huu kwa sababu hii ni kazi ambayo kila mtu anaweza kuifanya na inachohitaji ni wewe na computer yako na Internet connection, baada ya hapo ni wewe kutenga mda kila siku kujifunza namna ya kutrade, na kama nilivosema hapo mwanzo kama ukianza kujifinza kutrade forex 2020 mwezi wa kwanza au ukiwa serious na kuweka mda wa kutosha mwezi wa sita unaweza kuwa tayari kutrade live, ila kama kazi zikiwa zimebana sana basi mwezi wa 11 unaweza kuanza kutrade live account na kuanza kutengeneza faida.

Kuamua kutrade forex au usitrade forex mwaka huu 2020 hayo bado ni maamuzi yako, ila kumbuka kuwa hata kama wewe ni mmoja wa watu wadogo sana watakaokuwa wanatrade forex (Retail Trader) bado unaweza kupata faida nzuri sana kwenye soko la forex. 

Unatakiwa kujua ni watu gani wanahusika kwenye soko la forex na nini hasa kinafanya bei zinapanda na kushuka. Bank kubwa kubwa duniani, commercial banks, na makampuni zinauhusiano mkubwa sana na soko la forex na zinaweza kusababisha bei ikapanda na kushuka. 

Kama unataka kuanza kutrade Forex ni vema ukaanza tu na demo account ufanye mazoezi mpaka uelewe namna ya kutrade ndio udeposit hela yako utrade na kupata faida.

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x