Jinsi ya Kuanza Kutrade Forex 2021

Alright mwaka ndio unaendelea na ni kitu cha kumshukuru mungu wote tumevuka mwaka na mungu katujaalia, sasa je unajua Jinsi ya Kuanza Kutrade Forex 2021

Sasa ili u-survive kwenye hii dunia unahitaji vitu vitatu tu, chakula, maradhi au sehemu ya kuishi, na mavazi basi. Hayo magari, na mali zingine ni mbwembwe tu au unasemaje?  Sasa ili kupata hivi vitu tunahitaji pesa na  kuna njia nyingi za kujipatia pesa kama kuwa na kazi, au kuanzisha biashara. Ila kuna aina nyingine ya kujipatia pesa  na aina hii ni ya kipekee, Forex Trading. 

Forex trading ni njia ambayo watu wengi na hata mimi tunajipatia hela kwa kutrade kwenye soko la forex au forex markets. 

Sasa unaanzaje kutrade Forex? au jinsi ya kuanza kutrade forex 2021 inakuwaje?

Kitu cha kwanza bila kuyumba inabidi uanze kujifunza na kujua kwanza forex ni nini hasa na inaajumuisha vitu gani na inafanyaje kazi. Tambua kuwa kuna tofauti kati ya kuijua forex na kutrade forex. Unaweza kuwa unaijua forex ila ukawa huwezi kutrade. So kitu cha kwanza ijue forex kwanza na namna ya kuijua ni kutafuta google na kuangali videos youtube na kusoma vitabu na blogs kama hii yangu hapa. Usipoelewa zaidi ndio inabidi utafute mwalimu au mentors wakufundishe, japo siku hizi kuna semina nyingi zinazohusu forex so katika swala la kujifunza material yapo kila kona. 

Vitu vya kujua kwanza

Forex ni nini

Forex inafanyaje kazi

Mda wa kutrade forex

Na mtu wa kawaida kama wewe na mimi tunafit wapi kwenye hili soko la forex

Madhara ya kutrade forex

Mazuri ya kutrade forex

Mambo yoote hayo inafaa kuyafahamu kabla hujaanza hata kutrade. Uzuri ni kwamba hayo mambo unaweza kuyajua ndani ya weekend moja tu tayari ushayajua. Swala ambalo najua litakuchukua miaka na miaka ni namna ya kutrade forex. Hapo ndugu yangu ndio utakaa sana na hii itategemea na hapo mwanzo umeelewa au hukuelewa, ukivuka hiyo stage ukaanza kutrade moja kwa moja utaingia chakaa, ni kama unaanza darasa la nne akati la kwanza hukupita. So anza kusoma basics za forex kabla hujaanza kutrade ni muhimu sana kwa sababu kuna vitu vidogo vidogo unahitaji kuvifahamu wakati unatrade. 

Stage Ya Pili

Hatua ya pili kwenye namna ya kuanza kutrade ni kuanza kutafuta trading strategy utakayo itumia kutrade forex. Kama hujui trading strategy ni nini hamna shida, we click hapa nimeelezea vizuri kabisa, ila kwa ufupi trading strategy ni njia ambayo utaitumia kutrade forex, au ni namna ambayo utaitumia kutrade. So kuna njia nyingi sana au strategy wengine wanaita trading plan, ambazo watu wanatumia kutrade. Me natumia patterns, support and resistance vile vile price action na trendlines.  So baada ya kuelewa forex ni nini hatua ya pili ni kutafuta strategy yako utakayoitumia kutrade. 

Jinsi ya Kuanza Kutrade Forex 2020

Stage Ya Tatu

Hatua ni tatu tu. Hatua ya mwisho sasa ni Kufanya Mazoezi kwenye Demo Account. Practice Practice Practice. Kama unakumbuka nilisema kuijua forex haichukui mda ila kutrade forex ndio kuna chukua mda na kuna kazi kubwa,  na kazi yenyewe ni kufanya mazoezi kwa kutrade hiyo strategy yako mpaka uielewe. Me nimeanza kutrade forex mwaka 2015 na nimetumia miaka minne kujifunza kutrade na mwaka 2019 ndio nimeanza kupata profit kila mwezi angalau,  ila kabla ya hapo ilikuwa ni up and down mwezi huu na-win, mwezi huu na-lose sometimes miezi mitatu mfulurizo na-lose hela yote  mpaka naunguza account. So amini ninapokwambia fanya mazoezi ya kutosha kwa sababu kama unatumia strategy moja na ukaifanyia mazoezi kwa mda wa miezi mitatu mpaka sita na ukaona ina kuletea profit then deposit hela uanze kutrade live.

Stage ya Nne. 

Najua nilisema kuna hatua tatu ila nimekumbuka zipo nne. Hatua ya nne ni Kudeposit hela kwa broker na kuanza kutrade na real money au hela za ukweli ambazo unaweza kuzitoa na kwenda kununua mkate na kitoweo. 

Hatua hii sasa ndio ya mwisho ambapo baada ya kujua forex ni nini, ushatafuta strategy ya kutrade forex, ukafanya mazoezi kwenye demo account, sasa kinachofata ni kufungua real acount ambayo utadeposit hela yako wewe mwenyewe kutoka benk then unaendelea kutrade kwa kutumia hiyo strategy uliyoifanyia mazoezi na ukipata profit unawithdraw au kutoa hela na unaenda kuitumia. Thats it😎

Kwa Hiyo!!!

Kwa hiyo forex trading ni aina moja ya biashara ambayo unaweza kuifanya, na ikakuingizia shilingi mbili au tatu kwa week au kwa mwezi. Watu wengi wanaanza kutrade forex wakidhani ni kama mchezo tu, ila ukweli ni kwamba forex trading ni kama biashara zingine, unapoanza, anza kama vile unaanzisha biashara, kuna mambo unatakiwa kujifunza kwanza kabla hujadeposit hela yako, so, kwa sababu hiyo ni vema ukaaanza kujifunza kutrade mwaka huu kwa sababu itakuchukua mda mpaka ufahamu kutrade na kama ukianza sasa hivi na ukajituma, mpaka mwaka 2021 utakuwa mbali na unaweza kuanza kutrade na real money na kutengeneza pesa trading forex. So hujachelewa anza mapema ili mwakani uanze Ku-Crush The Market Like Craizei……

Cheers!!

0 0 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x