Ufanye Nini Unapo Lose Trade? Forex Trading

Najua ishawahi kukutokea unaingia kwenye trade baada ya nusu saa au masaa mawili unalose au una-close hiyo trade pips -50. Unafanya nini sasa baada ya hapo? Unalia, unabamiza computer ukutani, unanuna, au unakataa kula kabisa..hahaha. Me nakumbuka mwanzoni hadi hamu ya kula ilikuwa inaisha kabisa computer sitaki kuifungua kwa masaa kadhaa na nikifungua naangalia movies mpaka kesho na hamu ya kutrade inaisha. So baada ya muda na kuzoea kupata losses nikajikuta naweza kucontrol hisia zangu au emotions kila ninapo lose trade na kuna baadhi ya vitu nataka ku-share na wewe. 

Inabidi Uzoee Kupata Losses. 

Yap! Me huwa nasema losing is part of the game. Yaani katika akili yako ni unatakiwa uzoee kupata losses ili uweze kukomaa kiakili na kisaikolojia. Mwanzoni me nilikuwa nakosa hamu ya kula nikipata losses na nachukia hata computer kuiwasha, hiyo ni kwa sababu nilikuwa natrade na real money na nilikuwa sijazoea kupata losses ndio maana kila nilipokuwa nakosa trade nachanganyikiwa. Ila sasa hivi nishazoea kupata loss kiasi kwamba nikipata loss ya $100 bucks siwazi sana kwa sababu nimeshaelewa kuwa kupata loss ni sehemu ya kutrade. Ni kama biashara ukipata hasara leo, kesho hautafunga duka na kukaa nyumbani,utaendelea kwa sababu hasara ni sehemu ya biashara. 

Unapopata Loss Hakikisha Sio Kosa Lako. 

Hapo namaaanisha nini sasa?? 

Kila trader  ana strategy anayoitumia kutrade, kwa maana ya kwamba unajua conditions zako ni zipi, unajua unaangalia nini kabla ya kuingia kwenye trade, na unajua unaangalia nini wakati wa kutoka, vile vile unajua stop loss unaiweka wapi. So ukishaona trading set up ambayo inaendana na strategy yako ndio unaingia kwenye trade na kusubiri matokeo, na mara nyingi kwa kuwa umefata sheria za strategy yako utakuta losses unazozipata zinakuwa na MARKET imeamua kukufanyia mbaya na price  ikaenda  tofauti na plan yako kwa wakati huo. Me huwa nasema “The Markets Turned To Be a Stupid Idiot”. Kwa sababu set up yako inasema price inatakiwa kwenda juu alafu yenyewe inaenda chini huo si ni uchizi sasa! So stupid kabisa.

So ninaposema hakikisha loss unayopata sio kosa lako namaanisha kwamba fata sheria ulizojiwekea kwenye strategy yako ili unapopata loss usijilaumu kwa nini hukufata plan yako, matokeo lawama zibaki kwa market maker. Yaani kama wewe unaingia kwenye trade kwa kufata support and resistance areas au zones na unataka mpaka price iguse hiyo line ya support ndio uingie kwenye trade, basi fanya hivyo. Ila ukijichanganya tu ukaingia kwenye trade wakati price haijagusa msitari wa support alafu ukapata loss hapo utakuwa umejitakia mwenyewe.

Utasema market imekuchenjia wakati wewe hukufata sheria ulizojiwekea. Ni muhimu sana kufata sheria ulizojiwekea ili unapopata loss iwe ni kwa sababu market imeamua kuwa stupid idiot na ikakuchenjia badala ya kwenda juu yenyewe imeenda chini ila wewe uliingia kwa kufata sheria zako. Kama unapata losses zaidi ya wins basi fanyia marekebisho hiyo strategy yako. 

Relax, Tulia Punguza Emotions.

Ukishafata sheria za strategy yako na bado ukapata loss, kitu cha kwanza, tulia usianze kupanic na kupandisha hisia za ajabu ajabu. Ukiruhusu hisia au emotions ziingie ndio utapata mawazo ya kufanya revenge na kutaka kuingia tena kwenye trade bila kufanya analysis na ndio maana unashauriwa baada ya kupata loss zima computer toka nje kapunge upepo mpaka hisia zitakapo tulia ndio urudi kwenye trade.

Yaani subiri kidogo emotions au hisia zitulie ndio urudi kwenye computer. 

Hizi emotions au hisia yaani sijui nizielezeje ila yaani ni kama ile hali ya kuwa na kihasira flan hivi, yaani unapata kihasira kwa nn umelose so unatakiwa ukisimamie hiko kihasira kisiwekepo. Unajua hasira hasara kwa hiyo unatakiwa kupunguza hiko kihasira kikija ili utulie na kadri unavyozoea kupata loss ndio utazoea kukituliza, ila muhimu jitahidi kutuliza hizo emotions au hisia ili uweze kucrush it again.

Rudi  Na Uangalie Wapi Umekosea au Nini Kimesabisha Upate Loss. 

Baada ya kuondoka kwa mda na hisia zimeshatulia au emotions, rudi kwenye  computer na ujaribu kufanya analysis na kuangalia ni wapi umekosea au nini kimetokea mpaka ukapata loss, ukirudi utajua tu nini kimetokea je market imekuchenjia au ilikuwa ni

fake out au vipi. Kila trade ninayolose najitahidi kadri ya uwezo wangu najua kwa nn nimelose na nini cha kujifunza ili next time ikitokea kitu ka hicho najua nini cha kufanya.

Kwa Hiyo??? 

Kwa hiyo my friend, take point hapa ni kwamba kila unapopata loss kwanza relax, tulia, kama unaona kihasira bado kipo funga computer nenda kanywe maji na juice sio soda! Kunywa juice ni nzuri kwa afya. Baada ya mda rudi na uangalie nini kimetokea  na wap pa kurekebisha. 

Mimi sa hivi haki ya nani ninapopata loss najua markert imeniamulia na imeamua tu kunichenjia na kwa sababu ninakua nimeingia kwenye trade kwa kufata sheria nilizojiwekea basi naelewa kwamba hiyo loss ni makert maker tu kaamua kuwa Stupid so namuachia tu ila mwisho wa week nakua nime – Crush Like Craziiie😎😎

Kama umerisk 1% ya account yako basi huna haja ya kupanic kwa sababu hiyo ni rahisi kumanage. Ila ushauri mdogo atleast risk 0.5% ya account yako kwa kila trade hiyo ni nzuri zaidi.  

So ili kupunguza Panic:

Tengeneza rules au sheria ambazo utakuwa unazifata kila unapotaka kuingia kwenye trade

Fata sheria bila kupindisha

Loss ikitokea relax na upunguze kihasira….emotions

Kumbuka inabidi uzoee kupata loss ili ukomae so Man Up

Ukishindwa kupunguza kihasira funga MT4 kwa mda kidogo ukishindwa kabisa zima computer ukishindwa kabisa toka nje ya nyumba…….

5 1 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x