Aina Ya Traders, Tambua Wewe ni Trader wa Aina Gani

Kama ndio unaanza kutrade forex hiki ni kitu muhimu sana kukijua na ni  wewe unayetakiwa kufanya maamuzi kuwa unataka uwe trader wa aina gani. Hivyo kabla hujaanza ni bora kujitathmini wewe unataka kuwa trader wa aina gani.

Ni muhimu kujua wewe ni trader wa aina gani kwa sababu hii,  itakusaidia kuweza kupanga trading plan au strategy au mpango wako ili uweze Ku-Crush the Market Ile Mbayaaa

Aina Za Forex Traders.

Ujue hapa naongelea traders watu kama wewe na mimi kuna aina za traders yaani tunatofautiana na style zetu za kutrade ni tofauti, ila wote tunatrade kwenye aina moja ya market, Forex.                                                                                                                                                  

  1. Day Trader     

Huyu ni trader ambaye yeye anaingia kwenye trade ndani ya siku moja na anafunga trades zake ndani ya siku hiyo hiyo moja. Halazi trades mpaka kesho yake ye akiingia asubuhi jion ameshafunga. 

Kwa rugha nyepesi day trader ni kama mfanyabiashara wa kawaida ambaye anafungua duka asubuhi na kufunga jioni. So kama ukiamua kuwa day trader wewe utakuwa unatrade kila siku ya mungu na trades zako unaakisha unapoenda kulala hamna trade ambayo ipo open au iko on.

2. Scalper

Scalper a.k.a Scar Scaaaar……Me ni scalper by the way sometimes ila,  na  sisi scalpers huwa  tunaingia kwenye trade na kutoka kwenye trade ndani ya mda mfupi sana, mfano ndani ya nusu saa au dakika kumi na tano au masaa kadhaa. Yaani sisi in IN and OUT. So aina hii ya trader yeye anaingia na kutola mda mfupi tu. So ukiamua kuwa scalper wewe chart zako utakazokuwa unafanyia analysis ni 1Hr 30min 15min na wakati mwingine 1min. 

Uzuri hii aina unaweza kutrade mda wowote 

Kupata Profit Ni Rahisi Ndani Ya Mda Mfupi Utapata Wins na Vile Vile Ni Rahsi Kupata Loss, 

Ubaya Wa Hii Style ni kwamba.   wins unazopata zinakuwa sio kubwa saana kuliko day traders kwa sababu wewe movement zako zinakuwa ni za mda mchache sana so unaweza kujikuta unafunga trade mapema alafu price ikaendelea kwenda chini.

3. Swing Trader

Huyu ni trader ambaye anaingia na kukaa sokoni kwa mda mrefu na kulaza trade zaidi ya siku moja hata mbili tatu. So kama ukiamua kuwa swing trader wewe ukiingia kwenye trade unalaza mpaka kesho au keshokutwa ndio unafunga. So utakuwa unatrade long time trades na wakati wa kufanya market analysis unakuwa unaangalia timeframe kubwa za kuanzia za mwezi, week, siku 4hr hadi 1hr. 

Uzuri wa aina hii ya trader ni kwamba huhitaji kuwa kwenye charts kila siku na kila mara kuangalia trades na kufanya market analysis, unaweza kufanya market analysis jumatatu ukaeendelea na mambo yako mpaka labda alhamis huko unaangalia trade zinaendaje. 

Kitu kingine aina hii ya traders ukiwin unapata faida kubwa sana kwa sababu movement inakuwa ni kubwa kwa sabbau unakuwa unatumia timeframe kubwa za mfano 4HR, daily au weekly.

Ubaya wa hii style ni kwamba inachukua mda sana kusubiri profit au price ifikie target. We fikiria unaingia kwenye trade jumatatu yaani inabidi usubirie siku mbili mpaka alhamisi ndio price inaweza kufika kwenye target.  So kuna baadhi ya watu hawawezi kusuburia ndio maana wanaamua kuwa Scalpers au Day traders. 

4. Position Traders

Aina hii ya trader ni trader ambaye akiingia kwenye trade inakaa kwa mda mrefu sana kuanzia weeks, miezi mpaka miaka kadhaa. So kama ukiamua kuwa position trader wewe unaafanyia market analysis kwenye Monthly na wekly chart then ukiingia kwenye trade unatizamia kuifunga hiyo trade baada ya week nne au tano au unaacha miezi kadhaa ndio unaifunga.

Hii style huwa inatumiwa na Banks ila kwa sisi retail traders huwa tunaishia kuwa swing traders japo unaweza kuwa position trader ni wewe tu na unaruhusiwa.

 Mimi ni day trader na sometimes nafanya scalping, kuna baadhi ya  trades zangu nazifunga ndani ya siku na zingine naziacha zinalala na kuzifunga kesho yake.  Uzuri wa kuwa day trader ni rahisi kutrade mda wowote hata kama umebanwa na kazi bado unaweza kutrade. 

Sooooo Kazi ni kwako chagua ni aina gani ya trader unataka kuwa…… au unasemaje?

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x