Je Unaweza Kutengeneza Pesa Trading Forex Hata Kama Hujui Kitu Chochote Kuhusu Forex?

Hili swali watu wengi sana wanajiuliza na kushindwa kupata majibu, so nataka nikuambie jibu hapa hapa bila kuficha bila kupepesa macho. 

jibu ni NDIO  unaweza kutengeneza pesa kwa kutradde forex bila kujua kitu chochote………Subiri kwanza

Ninaposema bila kujua chochote sio uwe zero kabisa kuhusu forex, angalau uwe unajua basics tu za forex ujue hata forex iko vipi, unatrade vipi unapata hasara hiki ndio muhimu na vitu vingine vidogo vidogo. 

Ngoja nikuulize kuna biashara ngapi ambazo tayari umeshaaanza kuzifanya na wakati mwanzo kabisa ulikuwa hujui kitu chochote, au kuna vitu gani kwenye maisha yako ambavyo sa hivi unafanya ila mwanzon ulikuwa zero kabisa na hujui kitu?  ukiangalia unaweza kuta kweli kuna vitu vingi unafanya ila mwanzon ulikuwa hujui. 

Unajua hii ni kwa nini? Kwa sababu binadamu tumezaliwa na ule uwezo wa kujifunza kitu chochote humu duniani na kama Mwanadamu akiamua kujifunza kitu, hamna kitu kitakachomshinda kuelewa hata asilimia 70%. Kama ukijiambia na kuamua kweli unataka kujifunza kutrade forex, kweli nakwambia utaweza kutrade forex na kutengeneza pesa nzuri kila siku iendayo kwa mungu. 

Kwa sababu unaanza unaweza kuanza kutengeneza hela ndogo ndogo me huwa naziita baby money ni ndogo kama 5, 10 25 30 40 50 bucks kwa siku au hata kwa siku mbili. 

Utawezaje sasa kutengeneza hizo BabyMoney wakati hujui kitu. 

Kuna njia ya kwanza na hii ni muhimu kuliko zote.

Jifunze Kutrade Mwenyewe. 

Kama kweli umeamua na kusema “Nataka kutengeneza pesa kwa kutrade forex” basi unachotakiwa ni kuwa tayari kujifunza kutrade mwenyewe. Nakwambia kama ukijipa masaa mawili kila siku kupitia vitabu vya forex na kufanya mazoezi juu ya namna ya kkutrade ndani ya  mwaka mmoja utakuwa ushaanza kutengeneza vi dolla tano, kumi au hata ishiri na tano kwa siku. 

Watu wengi wanashindwa kuendelea kutrade forex kwa sababu moja tu, hawana uvumilivu kutulia na kujifunza vitu wanavyotakiwa kujifunza, na hii ni kwa sababu wakati wanaanza wanaichulia forex kama njia nyingine ya kujiingizia kipato wakati wewe unachotakiwa ni kuifanya forex kama biashara nyingine na utambue kwamba unahitaji elimu juu ya namna ya kutrade.

Hiki kitu cha uvumilivu nimejifunza the hard way na nakwambia umuhimu wa kuwa mvumilivu wakati unaanza kutrade. 

Kitu ninachoweza kukwambia ni kwamba Anza Mapema Kujifunza Kutrade Forex Na Uwe Mvumilivu. Haki nakwambia Me nimeanza kuijua forex mwaka 2015, nilikuwa bado nipo chuo, nikakurupuka sikuwa na uvumilivu nikaweka laki tano ikaisha yote ndani ya wiki moja, baada ya hapo nikawa nadeposit vidolla kumi, hamsini, vinakwenda bila faida yoyote,, hiyo yote nilikuwa sitaki kujifunza so nikawa natafuta shortcut, systems mpaka mwaka unaisha sijapata faida hata kidogo na hela nilizopoteza ni zaidi ya milion. Kupoteza milion moja wakati upo chuo kwa maisha yetu haya ya chuo lazima ulie, ila kwa sababu nilikuwa chuo nikasema huu ndio muda wangu wa kujifunza maana nikimaliza chuo sitakuwa na muda wa kujifunza so, niligive up mwaka 2016 wote sikutrade hata kidogo kwa sababu niliona kama forex sio kitu changu. Ila ile hela iliyopotea iliendelea kuniuma, huku naona watu wanatrade na kupata faida, mwaka 2017 ndio nikaamua kusema no matter what lazima nijue kutrade forex. So nikaanza upya. 

Kuwa mvumilivu ni kitu muhimu sana na unaweza ukawa unajua kutrade ila usipokuwa na uvumilivu utaunguza acccount kila siku. 

So Unawezaje kutengeneza pesa. 

1. Tafuta masaa yako mawili kwa siku uanze kujifunza kutrade forex. Me napendelea asubuhi sana, amka saa kumi mpaka kumi na mbili. na vile vile jioni kuania saa moja mpaka saa nne, huo ni mda tosha kabisa wa wewe kujifunza kitu kuhusu trading. 

2. Chagua pairs kama 5 tu za kuanza kutrade. Ukianza kutrade na pair nyingi zitakuchanganya jaribu kuanza na pair chache tu hasa major pairs kama EURUSD, USDJPY, USDCAD,GBPUSD,USDCHF.

3. Tafuta strategy ambayo unaweza kufanya mazoezi. Strategy ni njia ambayo utaitumia kutrade forex na hii ndio muhimu kwa hiyo kama trade unatakiwa kutumia muda wako mwingi kujifunza namna ya kutrade na kufanya mazoezi ya kutrade kwenye Demo account. Ndio maaana nasema ni vizuri ukaanza mapema kutrade. 

4. Ukishapata strategy yako endelea kuitumia hiyo hiyo wala usibadilishe badilishe strategy. Ukiendelea kubadilisha strategy unajichelewesha na unapoteza muda. Me nilikuwa napoteza hela kwa sababunilikuwa naruka ruka, leo ntarde strategy flan kesho naangalia youtube naona strategy nyingine naanza kuitumia hiyo, so mwisho wa siku nawasha computer nataka kutrade sijui hata nitumie strategy ipi maana nimejichanganya mwenyewe. 

5. Tumia money management. Kiasi unachorisk kwa kila trade kisizidi asilimia 1-2 kwa kila trade

6. Tengeneza plan yako na uifate. Traders wengi tunatengeneza plan asubuhi ila mchana saa nane tayari ushaharibu. Not Cool 

Njia Ya Pili Ni Kutumia Signal Providers. 

Signal providers ni mtu ambaye anajua tayari kutrade forex na anaelewa kufanya uchambuzi wa soko la forex. So yeye anachoksaidia wewe ni kukupa signals za kutrade ambapo wewe ukishapokea hiyo signal unaingia kwenye trade  na kusibir matokea kama itakuwa win au loss. 

Mfano wa signal utakuwa hivi

EURUSD BUY at 2550

SL. Stoploss at  2500

TP.  Take profit  at 2600

Kwa hiyo wewe kama trader kazi yako kubwa ni ukishapokea signals za aina hii ni kwenda kwenye mt4 yako na kuingia kwenye hiyo trade. 

Njia hii ya kutumia signals kwanza inakurahisishia kazi wewe kwa sababu wewe sasa hivi hujui kusoma charts na ndio kwanza unaanza kujifunza, ila  unataka kutengeneza pesaa,  kwa hyo cha kufanya ni kutumia signals utengeneze pesa wakati unaendelea kujifunza kutrade. 

Professional Traders wengi sana hapa Tz  na nje wanasema signals sio nzuri kwa sababu haujifunzi kitu kwa hiyo wanashaur kamwe usitumie signals ila ngoja nikwambie kitu. 

Lengo Lako Hapa Ni Kutengeneza Pesa Kwa kutrade Forex. 

Ila Hujui kutrade forex

Bahati nzuri kuna mtu anajua kutrade forex na anatoa signals na bei  ya dola 25, Na kenye account yako kuna dolla 100.

 Mfano, ukianza kutrade naye na akakupa signals nzuri na mwisho wa mwezi ukapata faida ya dolla 50 si unakuwa umetengeneza Pesa nzuri hapo, tena hujui kitu chochote.  

Kumbuka lengo lako hapa ni kutengeneza Pesa kwa kutrade forex, na sio kujifunza kutrade forex. 

So ni simple tu, ukweli ni kwamba signals wewe hutajifunza kitu, ila utatengeneza pesa. The point here is YOU WILL BE MAKING MONEY, Au ngoja niongee kwa kiswahili……

NI KWELI UKITRADE KWA KUTUMIA  SIGNALS HUTOJIFUNZA KITU ILA……….UTAKUWA UNATENGENEZA HELA AMBAYO UNAWEZA KULIPIA BILLS AU KULIPIA MTU AKAKUFUNDISHA NAMNA YA KUTRADE MWENYEWE. 

Its all about the money over here not learning. 

Ukitumia signals wewe lengo lako ni kutengeneza hela na kupata faida,  sio kujifunza namna ya kutrade. Pata hela kwanza ishike mkononi huku unaendelea kujifunza kutade mwenyewe. 

Kwa Hiyo?

So kama hujui kutrade forex ni kweli unaweza kutengeneza hela unachohitaji kama hujui KABISA KItu ni kuchukua mwezi mmoja tu kwaza ujifunze vitu basic vya forex mfano ujue forex ni nini na inafanyaje kazi na mtu anatrade vipi, ufanye mazoezi kidogo. Uzuri ni kwamba material za forex kwa kiswahili zipo nyingi sana kwenye mitandao na kwenye groups kwa hiyo, traders wengi wamejitahidi kutoa mafunzo bure kabisa kwahiyo ni wewe tu na muda wako ujifunze kutrade taratibu. Kama unamtaji mzuri tafuta signal provider mzuri uakupe signals ili uwe unatengeneza pesa huku unaendelea kujifunza kutrade mwenyewe. 

Cheers

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x