Ukweli Kuhusu Biashara Ya Forex…

Je Unajua ukweli kuhusu biashara ya forex? Watu wengi wanaoanza kutrade forex huwa wanakutana na mambo mengi na wanaambiwa na kusoma mambo mengi kuhusu forex. Kati ya hayo mambo mengi kwa bahati mbaya wanakutana na taarifa ambazo sio za kweli na mwisho wa siku ukijumlisha hizo taarifa zote unaanza kuona forex ni kama mchezo wa kubet au ni kama mchezo mchezo na sio biashara, so ndio nikaona niandike hii post kujaribu kuelezea hasa ukweli kuhusu biashara ya forex. 

Ukweli wenyewe kwa ufupi ni kwamba “Forex Trading” au Biashara ya forex kwa uhalisia kwanza tuanzie hapa, tunaposema na kutumia neno  “Biashara Ya Forex” sio kwamba wewe ukiamua kufanya hii biashara utaitwa wewe ni mfanyabiashara wa forex, hapana wewe utakuwa unaitwa “Forex Trader” au Investor au mwekezaji mdogo, mara nyingi utakuwa unaitwa Forex Trader, hii ni  kwa sababu  hamna bidhaa zozote utakazokuwa unanunua na kusema unatafuta wateja wa kununua, hapana hii ni aina au njia nyingine ya kujiingizia kipato kwa kutrade soko la forex. Forex maana yake foreign exchange, au kwa kiswahili rahisi ni ubadilishanaji wa fedha za kigeni ni kama wewe una hela za kitanzania na unataka hela za kenya so unaenda bereau de change wanakubadilishia kwa hiyo hamna bidhaa hapo ambayo utaishika mkononi. 

Sasa utajiuliza kwanini tunatumia neno “Biashara Ya forex” 

Hii ni kwa sababu watu wengi wanaihusisha forex trading kama mchezo wa kubet. Yaani mtu ukimwambia namna forex inavyofanya kazi moja kwa moja anafikiri ni mchezo wa kubet wakati kiuhalisia forex trading au biashara ya forex ni kitu tofauti kabisa na mchezo wa kubeti. Unaweza Kusoma Hii Post Hapa nimeeelezea vizuri tofauti ya forex trading na michezo ya kubet.  Kwa hiyo ili kuwafanya watu wajue kwamba forex trading sio mchezo wa kubet ndio maana tunatumia neno biashara, na ni kweli kwa upande mwingine unapoamua kuwa forex trader unatakiwa ujiambie kuwa unaanzisha biashara sio unacheza cheza tu, tuna msemo huwa tunasema “If you treat forex trading as a business you will make profits” Yaani ukiichukulia forex trading kama biashara utatengeneza faida. 

Je Forex Trading Ni Kama Mchezo Wa Kubet?

Hapana Forex Trading Sio Kama Mchezo Wa Kubet

Ili ufanikiwe na kuwa forex trader mzuri unatakiwa ujifunze namna ya kutrade, mimi nilipoanza kutrade ilinichukua karibia miaka mitano mpaka nilipokuja kuanza kutrade forex na kutengeneza faida, unajua hii ni  kwanini? Kwa sababu forex trading inahitaji ujuzi, inahitaji ujifunze, inahitaji mazoezi, na mwisho inahitaji usomee na kufundishwa ili uelewe namna ya kutrade au namna ya kufanya hii biashara kwa hiyo usifikiri ni kitu cha kuanza leo leo na ukafanikiwa kesho. 

Wakati mchezo wa kubet wala huhitaji kusomea kitu chochote, ni wewe tu na ndio maana unaitwa mchezo wa kubahatisha, forex sio mchezo wa kubahatisha, ni kitu ambacho kinahitaji ujuzi ili uweze kufanikiwa, ndio maana mpaka leo  hamna shule au sehemu yoyote inayofundhisha namna ya kubet ili ufanikiwe, ila kwenye upande wa forex trading kila kukicha unaona kuna watu wanatangaza wanatoa mafunzo ya forex trading hii ni kwa sababu forex trading au biashara ya forex ni biashara kweli ina inahitaji ujuzi ili uweze kutengeneza faida kila siku kuliko hasara. 

Je Ni Rahisi Kutengeneza Pesa Kwenye Biashara Ya Forex

Ndio, ni rahisi kutengeneza pesa vile vile ni rahisi kupoteza pesa

Trading forex unaweza kutengeneza elfu hamsini ndani ya saa moja,au ndani ya masaa manne, vile vile unaweza kupoteza laki moja ndani ya saa moja au masaa 24. Kwa hiyo kama trader unapotaka kuanza kutrade forex au kufanya biashara ya forex, usiichukulie kama mchezo mchezo, hii ni biashara ambayo hela inaweza kupotea ndani ya muda mfupi vile vile inaweza kupatikana ndani ya muda mfupi kuliko biashara zingine. Nakumbuka mara kwanza nilitengeneza dollar $10 ndani ya dakika tano, kipindi natrade binary options, vile vile kuna kipindi nilipo poteza laki nne ndani ya week moja.   Ndio maana tunaambiwa kwenye hii biashara inabidi utumie hela ambayo upo tayari kupoteza kwa sababu kama hujui unachokifanya unaweza kujikuta hela yako yote ikapotea ndani week moja.

Kwa hiyo ni kweli ni rahisi sana kutengeneza hela kwenye hii biashara ya forex ila unahitaji ujifunze namna ya kutrade kwa umakini ili utengeneza faida huku unalinda mtaji wako.  Kuna Msemo huwa tunautumia  “In Forex Trading Its Easy To Make Money and Easy To Lose Money!!”…… Kama ilivyo rahisi kutengeneza hela  kwa kutrade forex, vile vile ni rahisi kupoteza hela kwa kutrade forex….. 

Je Forex Ni Scam?

Forex sio scam. Uki-Click Hapa Nimeandika post inayoelezea Forex Tading Ni Nini unaweza kwenda kuisoma kwa kina. Ila kwa ufipi forex sio scam kwamba unaweka hela kwa broker na ukaipoteza na asikupe faida, hapana. Forex ni biashara halali na namna moja wapo ya wewe kupoteza hela ni kwa kutofanya uchammbuzi mzuri wa soko ukaingia kwenye trade na ukakosea matokeo yake ukapata hasara. Inaitwa hasara kwa sababu umekosea kufanya uchambuzi. Ndio maana unaambiwa kabla hujawekeza hela yako unatakiwa uwe umejifunza namna ya kutrade forex, uwe tayari una strategy nzuri umbayo umeifanyia mazoezi na umeona inaweza kukuletea faida, sasa ndio unaweza kudeposit hela yako na kutrade.

Ila kama hujui unachokifanya ni vema usiweke hela yako huko ufanye mazoezi kwanza. Watu ambao wanaongelea vibaya kuhusu forex trading ni wale ambao walidhani forex ni kama mchezo tuu unaingia kwemye trade na kutoka na faida, wakati hii ni biashara ambayo inahitaji wewe ufanye mazoezi usome, na kuelewa namna ya kulichambua soko la forex na kuingia kwenye trade na mpaka utoke kwenye trade, inahitaji ujuzi.  

Je Ni Lazima Kuanza Na Mtaji Mkubwa?

Hapana sio lazima kuanza na mtaji mkubwa.

Mimi mara ya kwanza niliaza na dollar $200 kama laki nne na nusu, ila kwa sasa unaweza ukaanza hata na laki mbili na nusu kama $100. Japo unashauriwa uanze na $250USD kama laki tano hivi. Kwa hiyo ukiangalia mtaji sio mkubwa sana unaohitajika, kinachohitajika ni wewe uwe unaelewa namna ya kutrade forex na una strategy ambayo itakuletea faida kila unapoingia kwenye trade huku unalinda mtaji wako. 

Kumbuka kwa kila biashara unapoanza na mtaji mdogo vile vile uwezekano wa kupata faida ndogo upo, kwa hiyo kwenye hii biashara ya forex unapoanza na mtaji mdogo, na faida zako zitakuwa ni ndogo kwa maana uwezo wako wa kutrade kwa kiwango kikubwa ni mdogo kwa sababu account balance yako ni ndogo. Kwa hiyo unahitaji uwe mpole na utambue kuwa  profit ndogo utazokuwa unatengeneza zitakupelekea wewe kutengeneza profit kubwa huko baadae. So usiwaze sana kuhusu ni shi ngapi utatengeneza kwa week, weka umakini kwenye kulichambua soko vizuri na kufanya market analysis vizuri ili usiweze kupata hasara kila mara, maana usipotapa hasara kila mara maana yake unapata faida. 

Forex Inachezwaje? Mtu Anachezaje Forex

Hii kitu naomba niseme kwa herufi kubwa FOREX HAICHEZWI NA HUU SIO MCHEZO, narudia tena FOREX HAICHEZWI NA HUU SIO MCHEZO. 

Forex ni kama biashara zingine inahitaji ujuzi na uelewa wa mambo hasa mambo ya finance. Kuna watu wengi sana wanadhani forex ni mchezo na ili utengeneze pesa inabidi ucheze kitu ndio utapata hela, kitu ambacho sio cha kweli. Forex sio kama mchezo wa kubet,  ni biashara unahitaji kusoma kujifunza na kuelewa namna ya kutrade forex kama hujui forex ni nini Soma Hii Post Inaelezea forex Ni nini. 

Kwa Hiyo??

Ukweli kuhusu biashara ya   forex trading kwa kifupi ni kwamba hii ni njia nyingine ambayo mtu anaweza kuitumia kama njia ya kujiingizia kipato, ni unapoamua kuwa forex trader unatakiwa uifanye kama vile unaanzisha biashara kwa sababu kama ukiweza vizuri na kuwa professional trader trading forex inaweza kuwa ndio njia yako kuu ya kukuingizia kipato na hata kuwa tajiri huko baadae. Ila njia ya kufika huko inahitaji ujuzi wa kufanya market analysis au uchambuzi wa soko na uvumilivu na uwezo wa kulinda mtaji wako huku ukikuza account yako taratibu. Huhitaji kuwa na haraka wakati unatrade forex, ni kuwa mpole huku unaendelea kujifunza namna ya kuongeza ujuzi wako na na winrate  yako. 

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x