Demo Account Ni Nini? Forex Trading

Kati ya vitu ambavyo mtu anapoanza kutrade forex anatakiwa kufanya ni kuanza kutrade kwa kutumia demo account ila demo account ni nini hasa? 

Demo account hiki ni kifupi cha Demonstration Account. Kwa kiswahili cha kawaida naweza kusema hii ni account ya mazoezi. Account hii inapatikana kwa kila broker na hii account lengo lake ni kukusaidia wewe unayeanza kutrade forex uweze kufanya mazoezi kwanza kabla hujawekeza hela zako. Account hii inakuwa na hela ambazo ni fake au bandia na hizi hela ndio ambazo utakuwa unazitumia kutrade na kufanya mazoezi kabla hujaweka hela zako na kuanza kutrade na real money. 

Hela ambazo zipo kwenye demo account huwezi kuzitoa au kufanya withdraw kwa sababu ni hela ambazo ni fake so zenyewe ni za kufanya mazoezi tu. Ukishaweza kutrade na ukaona uko tayari kutrade na real money ndio utalazimika kuwekeza hela zako ambazo kama ukitengeneza faida utaweza kuzitoa kutoka kwa broker mpaka bank

Faida za Demo Account

Kukupa Mda Wa Kujifunza

Faida ya kwanza ya hii account ni kukupa nafasi ya kufanya mazoezi na kuielewa hii biashara ya forex hasa kama wewe ndio kwanza unaanza kutrade. 

Yaani kama unaanza kutrade forex au uko interested na forex trading na hujui chochote kuhusu forex hii account haikwepeki yaani ni lazima uifungue ili ujue hii forex trading inafanyikaje. Kwa hiyo faida yake ni kukupa mda wa kujifunza forex trading.

Kufanya Testing ya Strategy

Kama hujui Strategy ni nini basi Soma Hii Post Hapa ila kwa ufupi strategy ni njia ambayo utakuwa unaitumia kutrade soko la forex, na hii njia utaipata kwa kusoma vitabu au kufundishwa. Sasa baada ya kufundishwa hii njia kitu ambacho huwa kinafata ni  kuifanyia kazi na mazoezi ili uielewe vizuri na hapo ndio demo account inapotumika. Hii demo account itakusaidia kufanya mazoezi na kufanya testing ya strategy ili uielewe vizuri. 

Unatrade na Live Markets

Ukiwa unatrade na demo account unakuwa unatrade na live markets. Hapa namaanisha nini?

Hapa ni kwamba live markets ambazo mtu mwingine atakuwa anatrade na real money au hela za kweli na yeye atakuwa anatrade hizo hizo markets ambazo wewe utakuwa unatrade tofauti tu ni kwamba wewe utakuwa unatrade na demo account na yeye anatrade na real  account ila conditions na vitu vingine mko sawa kwa hiyo ukija kudeposit na kuanza kutrade na hela za kweli utaendelea kutrade na live markets hiyo hiyo ulipoishia kitakachobadilika ni kwamba sa hiyo utakuwa unatrade na hela za kweli.

Demo account ni nini

Kwa Nini Ni Lazima Uanze Na Hii Account. 

Kwa Sababu Hujui Kutrade Forex

Kuna ulazima wa kuanza na hii account kwa sababu wewe unakuwa hujui kutrade. Kwa sababu hiyo inakulazimu uanze kutrade kwa kutumia hii account ili ujifunze namna ya kutrade na cha muhimu sana hapa ni kujua  namna ya kufanya market analysis maana market analysis ndio kila kitu na hapa ndio unakuta inabidi utumie hii account. 

Kujifunza Kutrade Forex Ni Rahisi, Ila Kufanyia Kazi Kitu Ulichojifunza Na Ku-Apply Ulichojifunza Kwenye Live Markets Ndio Balaa So Fungua Hiyo Demo Account Ufanye Mazoezi

Sasa ili kuepusha hilo balaa baada ya kufundishwa strategy na namna ya kutrade unatakiwa sasa ufanye mazoezi ya kufanya market analysis mpaka uielewe hiyo strategy na ukiona hiyo strategy huilewi unaacha unatafuta nyingine na ukiipata inabidi na yenyewe tena uifanyie mazoezi kwenye demo account na ukishaielewa ndio uanze kutrade na real money. 

Demo Account Inapatikana Wapi

Karibia kila broker huwa ana demo account kwa hiyo ni wewe tu kwenda kwa broker wako na utaona anademo account unafungua na atakupa log in details na utaanza kutrade risk free bila kuweka hela zako. 

Kwa Hiyooo???

Kwa hiyo demo account ni account ambayo inatumika kwa kufanyia mazoezi ya strategy mbali mbali. Wewe kama trader utaitumia hii account kufnaya mazoezi ni kama kwenda gym, hii ndi gym yako sehemu ya kujinoa na kutengeneza strategy ambayo utakuwa unaitumia ili ikuletee faida.  

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x