Faida Za Biashara Ya Forex

Biashara ya forex ni biashara kama biashara zingine. Kuna hasara na vile vile kuna faida.

Kwa sasa nataka niongelee faida za biashara za forex

Ni Rahisi Kuanza

Kwanza kitu unachohitaji kufahamu ni kwamba kuanza hii biashara ni rahisi kwa sababu hii biashara huhitaji vitu vingi kuanza. Unachohitaji ni Computer, Internet connection na mda wako wa kutrade basi, japo kuna swala la umeme wa kucharge computer ila hiyo najua sio tatizo sana. 

Sio Lazima Uwe Na Mtaji Mkubwa

Kwenye hili swala la mtaji watu wengi huwa wanabishana sana na kusema biashara ya forex trading inahitaji mtaji mkubwa sana ila kuna kitu inabidi tufahamu. Kwenye kila biahsara ukianza na mtaji mkubwa utatengeneza faida kubwa na ukianza na mtaji mdogo utatengeneza faida ndogo. 

Hii hali iko hivo hivo kwenye biashara ya forex trading. Ukianza na mtaji mdogo utatengeneza faida kidogo na ukianza mtaji mkubwa una uwezo wa kutengeneza faida kubwa, japo vile vile kama unajua kutrade unaweza kuanza na mtaji mdogo na ukatengeneza faida kubwa. 

Kwenye biashara ya forex unaweza kuanza na mtaji wa laki mbili na nusu au $100 USD na ukaweza kuanza kutengeneza faida kama za elfu ishrini au thelasini 15USD au hata laki moja kwa week. Kitu muhimu kabla hujawekeza hela yako ni muhimu sana uwe tayari ushajua namna ya kutrade forex la sivyo unaweza kuiweka hiyo laki mbili yako na ikaisha ndani ya week moja ukabaki unalia. So ni muhimu uwe unajua kutrade kabla hujawekeza hela yako. 

Ni Rahisi Kujifunza Hii Biashara

Kama hijui hii biashara inafanyikaje na hujui pa kuanzia, uzuri ni kwamba hii biashara ni rahisi kujifunza kwa maana ukitafuta information zozote zinazohusu hii biashara utazipata online, vile vile nashukuru hapa kuanzia mwaka 2019 hii biashara ndio ilishika kasi kwa hiyo kuna watu wengi sasa hivi wanaijua hii biashara na wanatoa mafunzo kila kukicha, ni wewe tu kufanya utafiti wako ni mwalimu gani unataka kwenda akufundishe ila kuhusu swala la kupata elimu juu ya hii biashara elimu inapatikana kila mahali kuanzia mtandaoni, mpaka mtaani. 

Kupata Faida Ni Haraka, Vile Vile Kupata Hasara

Faida kubwa kuliko zote kwenye hii biashara nikwamba kuna urahisi mkubwa wa kutengeneza faida na ni kwa haraka bila kutumia nguvu Hii ni. kwa sababu kazi zote zinafanyika online, wewe unachotakiwa ni kuhakikisha unajua kucham bua na kufanya market analysis ukishajua hivo basi kutengeneza faida inakuwa ni rahisi na  haraka. Hii inategemea na mda kuna baadhi ya trades ambazo utaingia unaweza kujikuta unatengeneza faida ya elfu hamsini au ishirini ndani ya masaa mawili  au manne au siku moja. Vile vile kwa mwenendo huo unaweza kupata hasara ya elfu hamsini au ishirini ndani ya masaa mwili au manne au siku moja. 

Kwa hiyo ilivyo rahisi kutengeneza faida haraka na kwa mda mfupi hivyo hivyo ni rahisi kutengeneza hasara ndani ya mda mfupi. Uzuri ni kwamba kuna kitu tunaita Money Management baadae ukijifunza hiki kitu, utagundua  namna ya kusimamia mtaji wako ili usipate hasara kwa haraka na kupoteza mtaji wako wote.  

Huhitaji Kufungua Duka Au Kuwa Na Ofisi Mahala

Hii biashara inafanyika kwenye computer au kwenye simu, kwa hiyo wewe kama Trader wa forex kama nilivosema huko juu utakachohitaji ni computer yako na internet connection na mda wa kutrade basi, kwa hiyo unaweza kuanza kufanya hii biashara nyumbani, ofisini hata barabarani mda wowote unaweza kuendelea kutrade Jumatatu mpaka Ijumaa. 

Una Mda Wa Kufanya Mazoezi Kabla Hujawekeza Hela Yako

Moja ya faida za biashara ya forex ambayo na yenyewe ni kubwa kabisa ni kwamba unaweza kuanza kufanya mazoezi kabla hujawekeza hela zako. Duniani humu hamna biashara ambayo unaweza kuanza kuifanyia mazoezi kabla hujawekeza mtaji wako, ila kwenye biashara ya forex trading hiko kitu kinawezekana. Ukitaka kuanza biashara ya forex unaweza kufanya mazoezi ili ujue hii biashara inafanyikaje, wakati biashara zingine huwezi kufanya hiki kitu zaidi ya kuwaona watu  wengine wanazifanya na ukawauliza maswali na wakakujibu, ila wewe kama ukitaka kujaribu lazima hela ikutoke. 

Kwenye biashara ya forex kufanya mazoezi  inawezekana kwa sababu unachotakiwa ni kufungua DEMO account kwa broker ambapo hii account inakuwa na hela bandia au vitual money ambazo utazitumia kutrade kama vile ungekuwa unatrade na hela zako mwenyewe. Kwa maana hiyo unapata mda wa kujifunza na kutengeneza strategy zako ambazo utazitumia kutrade pindi utakapoamua kuwekeza hela zako. So unaweza kuanza kufanya mazoezi sasa hivi na baada ya miezi mitatu ukishajua namna ya kutrade ukaweka mtaji wako na kutengeneza faida kwa sababu tayari ulishajua nini cha kufanya, kuliko biashara zingine unaweza kupata hasara kwa kitu ambacho ulikuwa hukijui. Biashara ya forex inakupa mda wa kutambua mambo yote unayotakiwa kujua kabla hujawekeza hela yako. 

Kila Mtu Anaweza Kuanza Hii Biahsara

Uzuri wa hii biahsara ni kwamba kila mtu anaweza kufanya hii biashara hata mtoto wa miaka 15 ukimfundisha anaweza kuifanya hii biashara kwa sababu kama nilivosema unachohitaji ni computter na internet connection na mda wa kutrade, kinachoongezeka ni ujuzi wa kutrade ukijua namna ya kutrade utatengeneza faida, ila kama hujui namna ya kutrade ndio utatengeneza hasara kila siku.

Kwahiyoo? 

So hii biashara ina faida nyingi sana na ni biashara ya kweli kama ukiamua kufanya hii biashara inahitaji uchukue mda wa kujifunza na kuielewa inavyofanya kazi. Kwa hiyo kama uko interested na hii biashara jipe mda wa kujifunza namna ya kutrade soma vitabu na utafute strategy yako ambayo utakuwa unaitumia kutrade na ukishajua kila kitu ndio ufanye deposit na utrade na hela za kweli ambazo unaweza ku-withdraw. 

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x