Cryptocurrency Wallet Ni Nini

Cryptocurrency wallet ni nini hasa? Hii ni Kama wallet za kawaida ambazo unaitumia kutunzia Cryptocurrency coin zako ambazo utazinunua. Ni sehemu tu ya kutunza fedha zako za Cryptocurrency.  Hizi wallets zinatumika kutunzia coin zako, kutuma na kupokea Cryptocurrency coin zako kama bitcoin au ethereum au ripple. Cryptocurrency coin nyingi zina wallet zake official na baathi yao wametoa maelekezo official ambayo yanaelekeza ni wapi utafungua wallets za kutunzia coin zao. Hawa inakua kwamba kama unataka kununua coin zao wana kampuni ambayo wanashauri uende ukafungue wallet kule ndio ununue coin zao. 

Ili uanze kutumia Cryptocurrency coin ni lazima uanze kwa kufungua wallet kwa ajili ya kutunzia coin zako. Ni kama wallet tu za kawaida. 

Cryptocurrency Wallets zinafanyaje Kazi?

Yaani iko hivi Cryptocurrency coin yenyewe kama bitcoin kwa mfano sio ambazo ndio zinatunzwa mle kwenye account yako bali kinachotunzwa ni Private Key. Private key ni kama pin code ambayo imeunganishwa na account yako ambayo ina idadi kamili ya coin ulizonazo. Kwa hiyo wallet yako inatunza Private Key au pin code na Public Key ambayo hii ni kama account namba yako ambayo unatumia kutuma na kupokea coin na inakua kama kitambulisho chako wewe na account yako.

 Cryptocurrency Wallet ipi sasa unatakiwa kufungua?

Mara nyingi unashauriwa kutumia official wallets za coin ambayo unataka kununua. Kwa hiyo kwa bitcoin nasahuri utumie Bitcoin core Wallet na kwa Ethereum tumia Ethereum Wallet au Myether wallet, kwa litecoin tumia Litecoin-QT.

Kuna wallets zingine ambazo ni universal unaweza kutunza coin zozote ulizonazo kama Holy Transaction ni moja ya aina hii ya wallets ambazo unaweza kutunza coin zozote ulizo nazo. Vile vile unaweza kutunza coins kwa kutumia exchangers kama Localbitcoins au binance na wao pia wana wallet za kila coin.

Aina za Cryptocurrency Wallets

Kuna aina nyingi za wallets kwenye ulimwengu huu wa Cryptocurrency. Kuna wallets za offline, online, desktop na paper. Kila aina ya wallet ina namna yake inavyofanya kazi na inatunza kiasi gani cha coin na aina gani ya coin unaweza kutunza. Kwa mfano Bitcoin wao wana desktop na mobile App.

Chini ni aina za Cryptocurrency Wallets ambazo watu wanatumia na unaweza kuangalia ipi inakufaa.

 1. Desktop Wallet
Cryptocurrency Wallet Ni Nini

Hii ni wallet ambayo inakua kwenye computer yako binafsi. Unadownload app kama software na inakua kwenye computer yako mda wote kwa hiyo coin zako unakua umezitunza hapo kwenye computer yako. 

Faida ya Desktop Wallet

 • Wewe ndio unaezitunza coin zako
 • Kama usipo-connect kwenye internet inaweza kuwa wallet nzuri sana

Hasara za Desktop Wallets

 • Ubaya wa hii wallet ni kwamba kama computer yako ikaharibika na kukataa kuwaka ndio umepoteza coin zako zote. Kwa hiyo kama ukiamua kutumia wallet hii hakikisha computer yako iko safe mda wote.
 • Kama ukisahau kufanya back up ya computer yako unaweza kupoteza coin zako
 • Kama computer yako imeharibika hakikisha unapeleka kwa fundi wa uhakika ukipeleka kwa fundi ambaye haeleweki unaweza kupoteza coin zako zote
 • Kama uki-connect internet unaweza kupata virus kwa hiyo amgalia site unazotembelea usiclick tu kila site unayoambiwa click.

2. Mobile Wallet

Cryptocurrency Wallet Ni Nini

Hii ni wallet ambayo ipo kwenye mfumo wa mobile application. So unakua nayo kwenye simu yako mda wowote

Hasara  za Mobile Wallet

 • Simu ni kifaa ambacho sio salama kabisa hamna kitu ambacho kitaweza kurudisha coin zako kama simu yako ikiweza kuvamiwa na virus
 • Simu yako ipo online na inakuwa wazi na rahisi kuingiliwa na virus so ni kuwa makini na website unazozitembelea

Baadhi ya Mobile Wallets ni kama

Jaxx

Breadwallet

Mycelium

3. Online Wallet

Cryptocurrency Wallet Ni Nini

Hii ni wallet ambayo ipo online na ni web based wallet ambayo unaingia kama unavyo-log in kwenye email address au online banking. Hapa hamna kitu cha kudownload kila kitu kinafanyika online tu. Kuna baadhi ya wallets zinakuruhusu wewe ndio uwe unaicontrol account yako na private key zako na kuna zingine wao ndio wanaokuwa in charge kwa hiyo ni vema kufanya utafiti kabla ya kuchagua ipi utaamua kutumia.

Faida za Online Wallets

 • Ni haraka sana kufanya muamala na transaction kwa haraka
 • Ni nzuri kwa kutunzia coin chache
 • Kuna baadhi unaweza kutunza aina mbalimbali za coin kama bitcoin na etherum kwenye account moja
 • Kuna privacy 

Hasara za Online Wallet

 • Wallet yako iko nje ya mikono yako yaani sio wewe ambae unamiliki wallet yako 100% kwa sababu zimetunzwa sehemu zingine.
 • Ni rahisi hackers kutuma virus na kuhack system za wallet na kupoteza coin zako zote.
 • Computer yako ipo at risk kwa sababu unaweza kupata virus malware,keyloggers viruses. Usiangalie wala kufungua websites ambazo huziamini na computer yako iwe na antivirus nzuri ambayo iko updated, na usitumie internet cafes au wireless wifi zozote usizoziamini. 

Baadhi ya online Wallets zinapatikana kwa exchnagers kama Bittrex, au poloniex, binance

Localbitcoins ni exchanger mzuri kwa hapa Tanzania na watu wengi wanatumia pamoja na Remitano 

4. Paper Wallet

Cryptocurrency Wallet Ni Nini

Hii ni wallet ambayo unaiprint kwenye karatasi QR code zote za Public key na Private key. Kwa hiyo hiyo QR code inatumika kama ndio kila kitu na unatakiwa kutunza hiyo karatasi kama mboni ya jicho lako.

Faida za Paper Wallet

 • Private key hazitunzwi  mtu mwingine ni wewe ndio unamamlaka yote na coin zako
 • Haitunzwi kwenye computer kitu ambacho kinaifanya hii njia kuwa ni salama zaidi

Hasara za paper Wallet

 • Inahitaji mda na ni kazi sana utakapohitaji kuhamisha coin kutoka mahala flan kwenda pengine
 • Pili inahitaji uelewa sana wa jinsi inavyofanya kazi. Kwa haiyo kabla hujaanza kuitumia ni vema ukaisoma na kuielewa vizuri jinsi inavyofanya kazi technically.

Mfano wa Paper Wallets 

BitAddress

Bitcoin Armory

5. Hardware Wallet 

Hii ndio wallet ambayo inasemekana ndio nzuri na bora zaidi kuliko wallet zingine zote. Hii wallet ni kwamba utatakiwa kununua kifaa kama USB  flash drive hiyo  inakua inakutunzia hiyo coin zako na kila ukitaka kutumia unachomeka kwenye computer kama unavyochomeka flash drive na kutuma na kupokea coin zako. 

Hii ndio wallet ambayo  ni salama kwa sababu wewe ndio unakua unatunza coin zako na hamna mtu mwingine aliyekushikia na kwa sababu coin zinapokua offline ndio zinakuwa salama zaidi kuliko zinapokua online kwa sababu kama hackers au mitambo ikisumbua coin zako zinaweza kupotea ila kama umezitunza offline zinakua salama zaidi. Mwaka 2014 Mt Gox Hack walifanyiwa hacking na wakapoteza coin zenye thamani Milion $460 USD.

Baadhi ya Hardware Wallet ni kama

Trezor 

Ledger Nano S

Hizi ndio wallets ambazo ni nzuri kwa wale ambao wangependa kununua coin na kutunza wakisubiri bei ipande ndio wauze.

Faida ya Hardware Wallet

 • Ni nzuri na salama kuliko wallet zote zilizopo
 • Ukiipoteza hiyo flash ndio umepoteza coin zako zote zilizokuwepo

Hasara ya Hardware Wallet

 • Ni ngumu kuielewa kwa watu wanaoanza kuitumia
 • Ni ngumu kupatikana mara nyingi unakuta ni mpaka uweke order wakutengenezee ndio unaipata labda ununue Amazon. Ledger amazon, TrezorAmazon

TIP: Unashauriwa 100% kama kweli unataka kutunza coin zako kwa mda mrefu ni vema ukazitunza offline na zisikae online. Either utumie hardware wallets au desktop wallets. Kama una hela ya kutosha nunua hiyo hard drive na utunzie coin zako humo na hii kama unataka kununua coin na kutunza kwa mda mrefu. Ila kama utanunua coin kwa ajili ya kutrade au kuuza ikipanda bei baada ya siku mbili basi sio lazima kutumia offline wallets but its best kutumia offline wallets kwa usalama zaidi. 

Sooo…

Likija swala la Cryptocurrency Wallets huwa hakuna nani ni bora kuliko mwenzie maana zote zina hasara na faida zake na za aina yake. Kwa hiyo ni wewe mwenyewe kama investor inabidi uamue coin unazotaka kununua utazitumiaje. Kama unataka kununua na kutunza kwa mda mrefu ili bei ikipanda ndio uuze basi nakushauri ujichange ununue hard drive wallets na kama unataka kununua coin na kuuza kesho kutwa bei ikipanda au kutrade basi tumia wallets zingine ambazo utaona inafaa. 

Tip: Unaweza kuamua kuzitunza coin zako kwa exchangers ni sawa pia ila ukae ukijua kuwa ni risk lolote linaweza kutokea kwa exchangers akavamiwa na hackers wateja wote mkapoteza coin zenu.

Ushauri Wangu.

Kwa upande wangu mimi nashauri hela ambayo utaamua kuitumia kuingia nayo kwenye maswala haya ya Cryptocurrency ifanye kama ni unaanza biashara mpya na uwe tayari kupoteza. Yaani naomba usichukue mkopo ukaweka huku maana bado hakutabiliki weka hela ambayo upo tayari hata ikipotea hauta yumba kichumi na ujaribu bahati yako. 

Nimejaribu kuelezea kwa urahisi hope umeelewa na kama hujaelewa uliza swali hapo chini kwenye comment na nitajibu kila comment thanks and lets make that money.

Cheers.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x