Umuhimu Wa Kutumia Stop loss. Je Ukitumia Stop Loss Ni Kujibana Au?

Kila ninaposema losing a trade ni kitu ambacho kila trader hakipendi, najua utakuwa unakubaliana na mimi. Ila ukiachana na hiyo kuna kitu kibaya sana zaidi ya kupata loss ya trade na unajua ni  kitu gani? 

Kupoteza Hela Zote Kwenye Account Na Kuunguza Account.

Ukipoteza hela zote na ukaunguza account ndani ya trade moja, hiyo itakuumiza sana mpaka utatamani aridhi ipasuke. Katika hali ya kawaida hii haitakiwi kutokea ila sometimes huwa inatokea na kama trader inabidi ukubaliane na hali halisi. 

Kuna kitu kinaitwa Stop Loss. Hizi stop loss wazungu walitengeneza kwa lengo la kumsaidia trader kama wewe na mimi tusiunguze account ndani ya trade moja, kwa hiyo kama unatrade na usipotumia stop loss, inamaanisha kwamba kuna uwezekano wa kuunguza account na hela yote ikapotea na ukapata hasara ndani ya dakika mbili. 

Stop Loss Ni Nini?

Stop loss ni kama mfumo ambao umewekwa kwenye hizi trading platforms MT4s na brokers ambapo huu mfumo unamsaidia trader kutumia kama njia ya kujikinga na kupata hasara wakati unatrade soko la forex. kwa kutumia mfumo huu wewe utakuwa unapanga ni shilingi ngapi uko tayari ipotee kama ikitokea trade yako ikawa ni loss na utapanga hii stop loss kwa kutumia pips kadhaa ambazo hizo pips ndio zitamaanisha ni kiasi gani kitapote. Ni muhimu sana kujua lot size unayotumia inamaanisha shilingi ngapi kwa kila pip.

Nini Kinatokea Kama Usipotumia Stop Loss.

Hii kitu iko hivi na traders wengi hata mimi wakati tunaanza huwa tunakosea. Me nakumbuka mwanzoni niliona kama stop loss ni kama kujibana. 

So mfano upo unaangalia chart na unatrade support and resistance strategy, price imefika kwenye resistance area na ikabreak hiyo area na kuendelea, Hapo sasa wewe ukajua kuwa sa hivi price ipo inatrend juu so ukaamua kuwa mpole na unatakiwa kuwa mpole na kuamua kusubir pullback, au retracement price irudi kwenye area hiyo ya resistance ambapo sa hiyo itakuwa na support na price ilivyorudi well hapo unakuwa na sababu ya kuinga kwenye trade. Ila bado unaamua kuangalia kama kuna news yoyote mda huo so unaenda inversting.com na kuangalia calendar na unakuta hamna news mda huo, Kitu kinachofata kuangalia price action hapo na engulfing candle hiyo hapo inatokea kinachofata ni kuingia kwenye trade na unapress BUY bila kuweka stop loss. Booooooom 

Umuhimu Wa  Kutumia Stop loss

Baada ya dakika 20 kweli trade ipo kwenye green na upo kwenye profit nzuri tu, so kwa kuwa uliacha kuweka stop loss kwa sababu zako mwenyewe na kwa sababu ulikuwa unaamini kwamba price lazima itaenda juu tu, unajua nini huwa kinatokea?………baada ya daikika 30 unashangaa kuna spike ya hatari hapo price inageuka na inarudi chini kama pips 200 na kuunguza acount yako yote. 

Kumbuka ulifata sheria zote za kuingia kwenye trade, trade iiikuwa inaonyesha kweli kuna uwezekano wa kenda juu ila trade  bado ikawa loss. Sasa kwa kuwa hukuweka stop loss iyo trade moja imekuunguzia account yote. Ila kama ungekuwa umetumia stop loss usingeweza kuunguza account yote. 

Kama  trader ukishapata loss ya aina hii huwa unafadhaika na kuvurugika. Nakumbuka trade yangu ambayo nilipata loss kwa kuwa siku weka stop loss ilinichukulia dola $60 zangu ndani ya dakika kadhaa na nikaunguza account chap na kwa kuwa ilikuwa usiku nikaamua kulala tu. 

Umuhimu Wa  Kutumia Stop loss

Kwa nini hii inatokea? 

Hii kitu mara nyingi huwa inatokea pale ambapo wewe kama trader unakuwa kama vile una uhakika wa hali ya juu, wazungu wanasema unakuwa Overconfidence na kujiamini kwamba soko ushalielewa na unajiambia kabisa trade hii lazima itakuwa good na hamna kitu kitakacho ingilia so unaona  hamna hata haja ya kuweka stop loss kwa sababu unaamini kwamba price lazima itaenda juu. 

Point ya kuchukua hapa kamwe usijiaminishe kwamba trade itakuwa na faida  hata kama kila kitu kinaonekana kipo sawa. Sio vizuri kwa afya yako

Unajua traders wengi wanaotrade bila kuweka stop loss wana ile kitu tunaita faidh au imani. Yaani wana imani kwamba trade itaenda tofauti na wao ila baadae itarudi tu na kuwa in blue na kupata faida ila baadae, hii hata mimi nilikuwa nafanya hivyo kwa sababu kama kweli unajua price ipo kwenye zone flan na unajua itarudi, kweli ukiweka stop loss itakubana na stop loss yako inaweza kuguswa alafu price ndio ikarudi.

Hivi unajuwa kuwa kama ukiwa na risk management nzuri unaweza kupata faida ndani ya trades 3 tu hata kama umepata loss 7 kati ya trades 10. 

Ngoja tupige hesabu chap hapa maana naona hatuelewani.  kuna kitu kinaitwa risk/reward ratio, hii inamaana kwa kila trade unayoingia unarisk $10 bucks na kama ukipata faida inapata $30 bucks hii ni kwa kutumia 1:3 risk/reward. 

Sasa kama umeanza kutrade na trades 7 za mwanzo zote zikawa ni loss, hapo utakuwa umepata loss ya $70 bucks kwa jumla. Ila ukaamua kukomaa na kuingia trades zingine 3 na hizi trade zote zikapata faida ya $30 bucks ambazo kwa jula ni $90 bucks. So ukiangalia hapo pamoja na loss zako saba bado umetoka na faida ya $20 bucks. 

Hii inamaanisha nini?

Kwanza kuweka stop loss ni kitu kingine na kitu muhimu ni kuhakikisha stop loss unaiweka kwenye maendeo ambayo ikitokea loss isikuumize sana na kukupa wakati mgumu kurudisha loss uliyopata. 

Guys losses zipo ila kama trader unatakiwa kuhakikisha kila loss unayoipata iwe rahisi kuirudisha na hapo ndio swala la kuwa na strategy moja ambayo unaifata na kuitumia na pili kuwa na risk/reward nzuri ambayo unaitumia kila wakati. Usichanganye madawa, kama ukinionyesha history ya trades zako ningependa kuona loss zako zinalingana au kupishana kidogo, sio loss moja umelose 20 ya pili 30 ya tatu 10 ya nne 40 ya tano 15 ya sita 70.,hiyo sio kabisa.  

Umuhimu Wa  Kutumia Stop loss

Kwa Hiyo??

Wakati naanza kutrade niliona kweli stop loss kama inanibana kwa sababu nilikuwa naamini kwamba niki press Buy na price iko kwenye support area, kweli itaenda chini kidogo alafu eti itarudi juu na kuwa in profit. Ukweli ni kwamba hii haiko hivyo, price inaweza kwenda chini zaidi au juu zaidi kuliko unavyofikiria wewe. Wazungu wanasema Never think the price is too high or too low” na kweli Kamwe usijaribu kufikiria kwamba price iko chini saaana au iko juu sana. Hii kitu nimejifunza the hard way, nakumbuka kuna trade ilikuwa chini saana a RSI illfika hadi kwenye level ya 15, hakika me nilijua hii price iko chini sana na lazima itarudi mda wowote. Nika buy kwa uhakika kabisa kwamba price lazima irudi juu kwa kuwa sababu eti niliamini kwamba iko chini sana, matokeo yake ndani ya dakika 30 naona price bado inashuka tu, ndani ya saa zima bado inashuka tu mpaka stop ikafikiwa. Kipindi hicho nilikuwa hata sijui maswala ya kuangalia chart kwenye higher timeframes so nilienda chakaaaa la hatari.

Kwa hiyo take point ni kwamba

– Tumia stop loss please please nakuomba tena tumia stop loss kwa kila trade unayoingia kwa sababu itakusaidia usiunguze account pale trade yako inapoingia Chakaaa.

– Unapotumia stop loss hakikisha pips unazoweka ni sawa na amount ambayo upo tayari ipotee. Piga hesabu kidogo kabla hujaingia kwenye trade. 

–  Zingatia risk/reward ratio. Kama risk/reaward ratio yako ni 1:1 jua kwamba kwa kila $10 bucks unayorisk ukipata faida utapata $10 bucks. Kama risk/reward yako ni 1:2 ni kwamba kwa kila $10 bucks unazorisk utapata $20 bucks kama ukipata profit. Hii ni muhimu sana kwa sababu itakurahisishia wewe kujua kwa kila loss utakayoipata itakuchua trades ngapi kurudisha hiyo loss na kuendelea kupata faida kila siku. 

–  Kubwa kuliko, weka stopp loss kwenye areas ambapo price ikifika kwenye hiyo area basi trading plan yote imevurugika. Hii kitu traders wengi sana wanachanganya.

– ‘Jitahidi sana  usifunge trade manually ni bora stop loss iguswe kuliko kufunga trade mwenyewe, utalia price ikirudi kulekule ulikokuwa umepanga iende alafu wewe ushafunga trade kwa sababu ya uoga wako. 

Traders wengi huwa tunaangalia amount ambayo tupo tayari ipotee na kusahau sehemu ambapo tunatakiwa kuweka hiyo stop loss.  Kwa hiyo unajikuta sehemu ambayo unaweka stop loss kweli ni amount ambayo upo tayari ipotee, ila sio sehemu ambapo price ikifika trading plan inavurugika, ndio maana unakuta unakuwa stopped out alafu price inarudi kule kule ulipokuwa unategemea price iende. Hii tunaita “Good Idea, Wrong Decision”

So tell me sasa we unaonaje swala la kutumia Stop loss je ni kweli kutumia stop loss ni kama kujibana au? Tell me in the comment …😎😎😎

Cheers

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x