Kwa Nini ni Lazima Uanze Kuweka Records Za Trades Zako. Trading Journal.

Ujue kuna kitu ambacho traders huwa tunakichukulia poa kabisa.  Sometimes huwa tunachukulia trading forex ni kama mchezo flan hivi ambao wewe kama trader kazi yako ni kusoma charts kuingia kwenye trade, kutoka na ku-withdraw hela na ku-spend hela then kesho unarudia process. Ila ukifata huu mlolongo kazini unapofanya kazi unakuta huwa unafanya kazi ila mwisho wa kazi unajua huwa kuna nini ambacho kila mfanya kazi hapendi kufanya? Kuandika Report. Najua unajua karibia asilimia 70 ya wafanya kazi duniani walioajiliwa hawapendi kuandika report ila kwa sababu BOSS anahitaji unalazimika kuandika report. 

By the way ngoja nikupe tips kidogo kwenye hili swala, kwa kuwa hupendi kuandika haya mareport na hasa huependi mtu akukumbushe kuhusu report, kitu ambacho mimi huwa nafanya ni kuandaa report mapema sana na kuituma kabla boss hajaiulizia. Huwa inaumiza sana boss akiulizia report so jinsi ya kumcrush ni kumpatia mapema hata kabla hajawaza kukuliza. 

Alright back to trading issues so kwa kuwa kazini huwa tuna report za kuandika, vile vile kwenye trading huwa tuna kitu kinaitwa trading journal, 

Trading Journal ni nini? 

Hii kwa ufupi hii ni kama report ya trades zako unazoingia wakati unatrade forex. Trading journal inaelezea vitu kama

Pair uliyooingia

Muda uliongia

Muda uliotoka

Matokeo

Strategy uliyotumia na sababu ulizotumia kuingia kwenye trade

So trading journal ni kama report yaani ile mwisho wa week ukiipitia ile report unajikuta unaelewa mwenendo wa namna unavyotrade na wapi pa kurekebisha.

Unapoanza kuweka record za trades zako kwanza inakusadia kuwa na displine kwa sababu unakuwa unajua namna unavyoingia trades zako na vile unajua wapi  ulikurupuka na wapi ulipatia. 

Hii inaweza kuonekana kama ni kazi rahisi ila traders wengi wanaanza kufanya hivi alafu baada ya mda wanaacha na kutegemea history ya trades za kwenye mt4. Trading history

Ishu ni kwamba trading history ya kwenye mt4 inakupa matokeo tu ya trades zako ila haikupi sababu kwa nini uliingia kwenye hiyo trade na kwa strategy gani ulitumia, na kwa nini ulitoka kwenye hiyo trade, kitu ambacho hizo taarifa hazikusaidii kwenye trade zinazofatia. 

Trading journal inakusaidia wewe kama trader kuelewa mwenendo wako na psychology yako juu ya namna unavyotrade. 

Ngoja Nikupe Mfano. 

Mfano wewe upo kwenye computer hapo na ukaona set up, trading plan yako inakwambia hiyo set up ni nzuri kusell, ila hisia zako na feelings zako zinakwambia hiyo trade haitakuwa na profit. So unajikumbusha na kusema “Sithani hii trade kama itakuwa profit ila inabidi nifate trading plan” so unaamua kuingia kwenye trade. 

Katikati ya trade price inaenda juu mpaka inakaribia stop loss yako kama pips 10 kabla iguse stop loss, hapa sasa unaaza kuwaza na kujiambia “Hii trade itakuwa loss na nilijua tu itakuwa loss sijui kwanini niliingia kwenye hii trade?” so unaamua kuclose hiyo trade hata kabla stop loss haijaguswa.

He!! Baada ya mda mfupi price inarudi kwa speed ya hatari na kwenda chinii zaidi kule kule ambako ulikuwa umepanga iende na kama usingefunga hiyo trade ungetengeneza profit nzuri sana.  Unaona eeh ishawahi nitokea na huwa inauma sana. 

‘Never close a trade manually ni bora stop loss iguswe kuliko kufunga trade mwenyewe utalia price ikirudi kulekule ulikokuwa umepanga iende.’

Ili hiyo hali isikutokee ndio maana unashauriwa kuwa na trading journal na kuweka records za trades zako kwa sababu  kama unarecords za hiyo set up unaweza kurudi na kuangalia ilikuwaje hiyo hali ilipojitokeza na kujua nini cha kufanya. 

TIP: Kama ulikuwa hujui kuna baadhi ya tools ambazo unaweza kuzitumia kurahisisha hii kazi ya kuandika journal. Hizi tools zinasaidia sana kujua namna unavyotrade na kujua acount yako inaendeleaje.

  1. MyFxBook
Trading Journal

Myfxbook ni website ambayo inachukua taarifa zote za account yako na kukupa full report juu ya account yako kwa ujumla. Mimi naitumia sana na inapunguza kazi, wewe kazi yako ni kuandika tu namna ulivyoingia kwenye trade na picha ya kabla ya trade na baada ya trade, ila mambo ya mda uliongia pips ngapi umepata drawdown ilikuwaje hivyo vyote unavipata ukiconnect account yako myfxbook.

2. FxBlue

Trading Journal

Fxblue na yenyewe ni website ambayo unaweza kuitumia ku-link account yako ipo sawa na mtfxbook na itakusaidia kujua perfomance nzima ya account yako kwa ujumla na namna kama uki-link account yako inakuwa rahisi wewe kujua account yako inaendeleaje na vile vile unaweza kushare report ya account yako kwa urahisi.

Ili hizi tools zifanye kazi kuna EA ambazo utadownload na kuinstall kwenye MT4 yako so instalation haichukui mda mrefu.

Kwa Hiyo?

Kwa hiyo me nasema kama kazini unavyoandika report, au kwenye biashara zako una taarifa ya mauzo na manunuzi, basi huo huo mwendo nenda nao unapokuwa unatrade. Huku kuna kitu kinaitwa trading jounal na kama trader unatakiwa kuwa na trading journal ambayo itakusaidia kuweka records zako za trades hasa kama bado unajifunza kutrade kwa sababu kama huweki records za trades zako hapa ndio utajikuta unaruka ruka na strategy mbali mbali kwa sababu unakuwa hujui strategy inafanyaje kazi, ila kama ukiwa unaweka records na unatumia jounal basi unakuwa unajua kama strategy inafanya kazi au vipi. So kama hutumii ni vema ukaanza mapema.

Cheers 😎

We unatumia journal au unatrade kimya kimya? Tell me in the comment…😎

4.3 3 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x