Tofauti Kati Ya Technical Analysis Na Fundamental Analysis.

Demo account ni nini

Kama wewe ni mmoja wa watu amabo unataka kuwa forex trader,  kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kufanya ni kutengeneza strategy yako jinsi utakavyokuwa unatrade na kazi kubwa ni kuipata hiyo strategy. Strategy hiyo inabidi iendane na style yako ya kutrade, risk management, na profit target. Sasa ili uweze kuwa na strategy nzuri ibidi uwe na uwezo mzuri wa kufanya uchambuzi wa soko au kufanya market analysis.

Aina za Uchambuzi wa Soko La Forex Market 

Kuna aina 3 za uchambuzi wa soko ambazo zitakusaidia kuchagua na kuangalia ni ipi inakufaa wewe. 

1. Fundamental Analysis

2.Technical analysis

3. Sentiment analysis

Fundamental Analysis

Aina hii ya uchambuzi kama trader unakuwa unafanya uchambuzi wa siko kwa kuangalia mambo ya uchumi, kisiasa, kijamii na namna yanayochangia kwenye soko la forex hasa kwenye upande wa supply and demand, na kuangalia madhara yatakayotea baada ya kitu flan kutokea. Mfano mzuri ugonjwa huu wa corona ulipotokea mwaka 2020 mwezi wa tatu pair nyingi zilishuka na Selling opportunity zilikuwa ni nyingi kwa sababu tu ugonjwa huu ulisababisha biashara nyingi kufungwa na matokeo yake mambo mengi yalisimama kuliko kawaida. Kwa hiyo kwa mtindo huu kama ulikuwa unatrade hapa ilikuwa ni ku-sell tu kalibia pair zote.

Technical Analysis

Aina hii ya analysis kama trader utakuwa unafanya uchambuzi wa soko kwa kuangalia price movement au bei ya soko kwa kutumia charts na kuangalia trading opportunity. Hapa ndio utaangalia na kutafuta strategy yako namna ya kusoma charts. Traders wengi tunatumia aina hii ya uchambuzi. Uchambuzi wa soko kwa kutumia technical analysis kwenye charts. 

Sentiment Analysis

Aina hii ya analysis wewe kama trader utakuwa unatrade kwa kuangalia tabia za watu na kuzielewa tabia zao na mienendo yao ikoje na kujaribua kuangalia mood ya traders wengine ikoje na inaadhiri vipi soko. Ila kama hujui watu ndio wanafanya soko la forex liendelee kuwepo na bei ziendelee kubadilika kila kukicha. Kwa hiyo wewe kazi yako ni kujaribu kufikiria kama watu sasa hivi wote wanasell na kiakili wameshapanic na ukiangalia price inaelekea kwenye support area wewe utakuwa unajua kwa traders wengi wataanza kufunga trades zao na kuifanya market ianze kwenda juu so hapo ndio unapata chance ya wewe kuingia kwenye trade. Hii naweza sema ni aina ya uchambuzi ambao unajaribu kusoma akili za watu na wanavyofikiria ili upate trading opportunity.

Aina ipi ya Uchambuzi Wa Soko Ni Nzuri. 

Traders wengi huwa wanajiuliza ni aina gani ya uchambuzi wa soko ambayo ni nzuri zaidi, na ukiangalia hili swali kulijibu ni vigumu kwa sababu kwa upande mwingine unajikuta unatakiwa kuchanganya aina zote za uchambuzi wakati unatrade.

Watu wengine wanasema huwezi kutumia technical analysis bila kuanza na fundamental, na wengine wanasema kama wewe unapendelea kutrade bila fundamental sawa na kama wewe unapendelea techinical analysis ni sawa pia. Ila kadri unavyoendelea kutrade utakuja kugundua kuwa hizi aina mbili zote utakuwa unazihitaji na kuzitumia zote kwenye strategy yako. Kwa traders wengi huwa tunatumia Technical analysis tunachanganya na fundamental analysis na kuangalia news gani zitaleta mchanganyiko kidogo kwenye soko ila kwa ujumla wengi tunatumia technical analysis.

Sasa kuna kitu kinaitwa News.

News unajua ni taarifa tu, ila sasa kwenye soko la forex kuna baadi ya taarifa ambazo zikitoka tu, huwa zinapelekea price kuvurugika na kutokuwa na mwelekeo wowote, kwa kitaalamu zinaongeza volatility in the market so kama ulikuwa umefungua trade na news ikatoka unaweza kujikuta unapata hasara kwa sababu hiyo news ilikuwa na impact kubwa kwenye soko. So kwa sababu hiyo zinazofanya traders tunachanganya fundamental analysis na technical analysis. Hii ni kwa sababu sometimes news zinafanya market inavurugika kwa hiyo kama trader unatakiwa kuhakikisha unajua ni mda gani news itatoka na ikitoka pair gani itakuwa affected  na ni namna gani ya kuitrade au unaacha kuitrade hiyo pair kwa mda mpaka market itakapo tulia. 

Mara nyingi news ikitoka  price huwa zinatembea kwa kasi zaidi na kuvurugika ila baada ya mda mchache zinatulia na kuwa kawaida, so ni kitu muhimu kukifahamu

Sooooo kuna tofauti kati ya fundamental analysis na technical analysis ila kwa traders unaweza kuchanganya analysis zote ili uweze kupata faida nzuri. 

Hii kitu ni wewe tu kuamua ni ipi unaipendelea zaidi, ila wengi huwa tunatumia technical analysi na fundamental, kam aunavoona watu wengi wanatumia charts kutrade so nina uhakika na wewe utakuwa unatumia hii style

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x