Namna Ya Ku-Control Emotions Wakati Unatrade

Trading forex kuna mambo mengi sana yanaendelea nyuma ya pazia. Yaani kuna tofauti kubwa kati ya mama muuza maandazi pale nje na wewe forex trader. Mama muuza yeye anachohitaji ni unga na viungo vingine apike na kuweka bidhaa yake hapo nje barabarani wateja wanakuja wananunua mpaka mchana bakuli limeisha. Akipata hasara maandazi yamebaki anakula yeye na familia anawapa majirani siku imeisha. Ratiba hii inajirudia kila siku na ukiangalia hana mambo ya kuangalia leo soko likoje, hawazi akipata hasara atapanic au vipi na mara nyingi kama anajulikana kila siku maaandazi yanaishaga so kila siku yeye ana faida. 

Tukija kwako sasa trader ndio kuna mabalaa. Mimi huwa nasema forex trading ni kama kwenda kuwinda myama porini, kila siku  ina vitu vipya. Kwenye soko la forex price inaenda juu na chini na hakuna bidhaa unayouza, ni hela yako tu ipo kwenye account na kazi kubwa uliyonayo ni kutrade hiyo hela ili upate faida, na kwa sababu soko linaenda juu na chini kuna kupata hasara na hapo ndio emotions au hisia au kihasira flan hivi me nakiita kinakuja na kukuvuruga. 

Unajua wewe kama trader akili yako inabidi iwe na uwezo wa kuvumilia mambo inayokutana nayo kwanza kuna  kupata faida na baada ya mda mfupi unapata hasara ndani ya mda mfupi, kwa hiyo akili yako na ubongo na mwili inabidi ziwe na uwezo wa kusimamia hiyo pressure na  wewe kama trader unatakiwa kujua namna ya kushusha hisia zako wakati zinapanda. Hatua ya kwanza kama trader ili uweze kuwa na psychology nzuri wakati unatrade  ni kuhakikisha unaweza ku-control emotions zako, ukifanikiwa hilo lazima ufike mbali na uta crush the market Like Craizeeee🤜🤛🤙😎

Sasa Vitu Gani Vya Kufanya Ili Kukusaidia Kutuliza Emotions.

Fanya Market Analysis Vizuri. 

Guys kuna kufanya market analysis, na kufanya market analysis vizuri. Hii namaanisha chukua mda kuiangalia pair moja baada ya nyingine na kufanya uchambuzi wa kina. Hii ni kuanza kuangalia timeframe kubwa za weekly unashuka daily mpaka 15 minute. Hii ni muhimu kwa sababu ikitokea umepata loss ni rahisi kuelewa kwa nini umepata hiyo loss na utajua wapi pa kurekebisha. 

Fanya Risk Management Vizuri. 

Hii kitu ni muhimu sana na narudia tena. Risk management ni kuhakikisha amount unayoweka kwa kila trade ile stop loss iwe ni asilimia moja ya balance nzima ya account. Hii ni kwa sababu kama account yako ina 100 na ukaingia kwenye trade risk ikawa ni asilimia mbili that means ukipata hasara itakuwa umepoteza 2 usd. Katika hali hii emotions haziwezi kuja kwa kasi sana na kukufanya ukapanic sana. Ila sasa kama uliweka risk ya 10 usd na ukapata hasara hapo lazima uvurugike kwa sababu balance itakuwa ni 90 usd. Yaani kupoteza 10bucks kwenye trade moja ni hasara kubwa hasa kwa account ya $100 usd. 

Risk Amount Ambayo Uko Tayari Ipotee. 

Tumia Stop Loss

Kuna traders ambao wao hawapendi kuweka stop loss kwa sababu eti inawabana. Guys mimi nilichojifunza stop loss haikubani, ila inakusaidia kulinda trade na mtaji wako usipotee gafla. Vile vile unatakiwa kuweka stop loss kwenye maeneo ambayo unajua kabisa price ikifika kwenye

hilo eneo basi hiyo trade imevurugika kabisa. So kama wewe unaamini stop loss inakubana well, sikulazimishi, ila kwa ninavyojua kalibia silimia 60% ya traders wanatumia stop loss.

Kubali Kupata Loss Ni Kawaida. 

Kitu cha kingine ambacho naomba uweke akilini mwako kila siku ya mungu ni kwamba, Kupata hasara ni kawaida kwa kila biashara. Mimi huwa najiambia losing a trade is part of the game. 

My friend unavoendelea kutrade unatakiwa kujua kuwa utakuwa unapata loss na inabidi uzoee kupata loss na inabidi ujue kuwa loss ni sehemu ndogo tu ambayo ulikosea so unachotakiwa ni kujifunza na kuendelea ku-trade. Ndio maana tunashauriwa kama small traders tuwe na strategy moja tunayoitumia na kuifata na ku-manage risk ili unapopata loss iwe rahisi kurudisha kwa sababu kwanza risk uliyotumia ni ndogo, na pili strategy yako ni nzuri so kama umepata loss moja kwa kuwa strategy yako ni nzuri hiyo loss itarudi na faida juu.

Sooo…

Kwa hiyo emotions au hisia kuna baadhi ya vitu wewe kama trader unatakiwa usivifanye ili usijileteee emotions za ajabu ajabu ambazo utashindwa ku-control, na ni vitu vidogo vidogo tu kama risk management, fata sheria ulizojiwekea, angalia news kabla hujatrade nakadhalika. 

Hizo ni baadhi ya tips ambazo ukiweza kuzitumia zitakusaidia sana ku-control emotions zako wakati unatrade kubwa kuliko risk management kwa kila trade hakikisha una-risk atleast 1% hii kitu ni muhimu na ni sababu kubwa watu wana-panic wanapopata hasara kwa sababu wame-risk hela nyingi kuliko account  balance yao, so ni wewe tu kuzingatia.

Cheers

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
error: Content is protected !!
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x